- Ni wapi vyombo vya habari vilipaswa kusimamia, kwa swala hili la kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa mgogoro kati ya serikali na Madaktari . Vyombo vya habari vinapaswa kuwaelimisha wananchi ni namna gani ya kujua nini haswa ni muhimu kwao, badala ya kujikuta wakiingia katika mabishano na mamlumbano yanayoashiria kufurahia “Ubabe” wa wanasiasa vs madaktari.
- Kwa sababu bila wananchi kuwapa pressure hawa, wao (serikali na madaktari) wataendelea tu na huo mgogoro kwa gharama yetu – yaani sisi wenyewe tunaowashabikia (ama kwa kuchochea madaktari, au kwa kuchochea serikali).
- Nina pata wasi wasi kidogo kwamba Magazeti, na watu wengi kwenye mitandao “social networks”, yakitokea matatizo, wanakua sehemu ya tatizo kwa kuongeza mafuta kwenye moto kwa mijadala ambayo mingine haina maana. KWASABABU KATIKA HILI, HAIJALSHI UKO UPANDE GANI, WOTE TUTAUMIA.
- Hata tukisema wafukuzwe, au tukisema waendelee kugoma, TUTAUMIA TU!
- La muhimu ni kuzibana pande zote mbili yaani serikali na Madaktari watueleze vizuri kwa nini wameendelea kung’ang’ania yao binafsi bila ya kuufikiria sisi na je ni kweli huwa wanatufikiria sisi....... sio tu kusema wako tayari kwa majadiliano kama vile suala hili halina uhitaji na umuhimu na wa haraka.
- Kwani Vyombo vya habari, vilipaswa visiishie tu kuripoti tu: “serikali imesema wameshindwa kuafikiana…” au “madaktari wamesema wameshindwa kuafikiana…” Ilibidi vyombo vya habari viendelee kudadisi ili kukosoa kauli zao wote, na kwa kufanya hivo yawezekana vyombo vya habari vingekuwa wa kupeleka kwenye suluhu au makubaliano ya kudumu ya mgongano huo.
- Unajua haitoshi tu kuripoti kuwa serikali au madaktari wamesema wako tayari kwa majadiliano, bila kuwauliza haswa ni hatua gani wanafanya kuhakikisha majadiliano yanakuwapo.Na isiishie hapo tu, pia tuangalie ni nini kitakachofuata pale mgogoro utakapoisha…!
- Upande mwingne tujiulize tunashughulika vipi na viongozi ambao wamekua ni wabadhilifu katika matumizi kwenye sekta ya afya? Tunawabaini vipi madaktari walioshiriki katika wizi au upotevu wa kizembe wa madawa au vifaa vya hospitali?
- Halafu na sisi wananchi wengine tujiulize je, ….Hakuna miongoni mwetu tuliouza vifaa vibovu hospitalini na leo tunawalaumu wanasiasa au madaktari?
- Lakini vipi ukiangalia kwa jicho la pili: “kiuchokozi”: Hivi wanasiasa wanaotupiana mpira katika hili suala, mara CCM, mara CHADEMA nakadhalika… kwa sasa wanatibiwa wapi? Ni jambo lisilo na kificho kuwa, idadi kubwa ya hawa wanasiasa ( bila kujali vyama vyao) wana “madaktari wao maalum/binafsi” au “vituo maalum” kwa ajili ya kuangalia afya zao na familia zao.
- Kwa upande mwigine , ndugu zetu, rafiki zetu madaktari - ni wangapi wana wateja maalum ambao ni wanasiasa hao hao waliovuruga mifumo katika sekta ya afya? Je, wanagoma kuwatibia hawa wakienda katika clinics zao binafsi? Hawa huitwa “Special clients” ambao ni hao hao viongozi, ambao leo wanawatuhumu ni chanzo cha huduma mbovu?
- Ni wazi kuwa Vyombo vya habari havijalichukulia swala hili kwa uzito unaostahili na kulifanyia kazi ndani nje nje ndani na matokeo yake, sisi wananchi, baadhi yetu, tumeamua kubandika lawama au kutetea upande mmoja kati ya pande hizi mbili, bila kujua kwa kufanya hivyo, TUNAJIUMIZA WENYEWE!
Friday, July 6, 2012
Wanafunzi TANZANIA E. COLLEGE tunajiuliza....
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment