Wednesday, January 20, 2016

MUHULA MPYA 2016

Heri ya mwaka mpya na hongereni kwa kumaliza mwaka 2015 salama, tunawkaribisha wote Tanzania Education College kuungana nasi katika muhula mpya wa mwaka 2016, tunaanza kutoa mafunzo katika kozi zetu tunazozitoa hapa chuoni. 
Zifuatazo ni Kozi zinazofundishwa hapa kwetu kuanzia Januari hii: 
-Business Admistration
-Human Resources 
-Clearing and Forwarding
-Journalism 
-Broadcasting
-Hotel Management
-Nursery Teachers
-Law
-Computer..
Tumeboresha mafunzo yote tunayoyatoa na tumeongeza wahadhiri wenye uwezo mkubwa wa kufundisha na kueleweka vizuri na wanafunzi.
Ada zetu ni zile za awamu zilizopita na wanafunzi wanaweza kulipa kwa awamu kwa uwezo aliokuwa nao,  tunafanya hivi ili kila mtu aweze kupata elimu kutoka kwetu. Pia chuo chetu kinatoa ngazi ya Astashahada  na Stashahada, kwa Stashahada tunatoa mafunzo ya miaka miwili na kwa Astashahada ni mwaka mmoja ingawa pia huwa tunapokea wanafunzi wenye matokeo mabaya kabisa kwa ajili ya kuwapa uwezo wa kujiunga na ngazi za juu.
Baada ya kumaliza masomo chuo kinawatafutia field wanafunzi wote watakao kuwa wamehitimu.
Ajira ni lazima kwa kila mwanafunzi atakayefanya vizuri katika masomo yake.

Tunawakaribisha wote kujiunga nasi kwani nafasi ni chache.

Imetolewa na
Mary Lucas Mfinde.
Afisa Uhusiano,
TANZANIA EDUCATION COLLEGE