Wednesday, July 25, 2012

WAHI FOMU ZA KUJIUNGA NA CHUO KWA PUNGUZO KUU LA ADA

Zikiwa zimesalia siku chache hadi kufikia mwishoni mwa mwezi huu wa saba ambapo usajili rasmi wa wanafunzi wapya kujiunga na chuo utafungwa, chuo chetu cha TANZANIA E. COLLEGE kinawakaribisha wanafunzi wa siha zote kuja kujiunga ili kurahisishiwa suala la ajira kama muhula na kaulimbiu yetu isemavyo, SULUHISHO LA AJIRA, fomu zimeshaanza kutolewa kwa bei punguzo ya shilingi elfu kumi ambapo kwa hiyo hiyo elfu kumi utapatiwa kitambulisho cha chuo, usajili kamili, mafunzo ya kompyuta na vitendo, mawasiliano na pia uanachama wa chuo kamili, ufaulu huzingatiwa hapa chuoni ingawa kipaji ndio kitu kikuu ambacho chuo huangalia katika udahili wa wanafunzi wapya, ada hutofautiana kulingana na kozi ambayo mwanafunzi husika anaisoma, kwa jinsi mpangilio wa chuo ulivyo kwa muhula huu ni kwamba, itapofikia mwezi Agosti kutakuwa na ziara KUBWA ya kimafunzo kuelekea bagamoyo na pia katika ziara hiyo kutakuwa na kuhudumiwa kwa kila kitu na chuo ila tu mwanafunzi atachangia kidogo, tunawakaribisha wote kwa ajili ya kubadilisha mlolongo wa maisha yenu.
IMETOLEWA NA MKUU WA CHUO,
TANZANIA E. COLLEGE.

Monday, July 23, 2012

CHRISTOPHER KOMBA, MOJA YA TUNDA YA TANZANIA E. COLLEGE

Kijana wa TEC akiwa anawakilisha uzuri sana huko Songea ndani ya JOGOO FM, kwa wale wanaokuwa maeneo ya Songea wasisite kumdaka hewani na kipindi cha Hali ya Hewa pia DIRA ZA KIMATAIFA.
Kaz ni kaz, haujalishi hata kuduwaa katika kujiandaa na kipindi kijacho.
Kijana Kazini, siye wana TANZANIA E. COLLEGE twamtakia swaum njema!

EDDIE MURPHY AFARIKI DUNIA

Actor Eddie Murphy is reported to have died shortly after a snowboard accident earlier today - July 24, 2012.
  The actor & novice snowboarder was vacationing at the Zermatt ski resort in Zermatt, Switzerland with family and friends. Witnesses indicate that Eddie Murphy lost control of his snowboard and struck a tree at a high rate of speed.

Eddie Murphy was air lifted by ski patrol teams to a local hospital, however, it is believed that the actor died instantly from the impact of the crash. The actor was wearing a helmet at the time of the accident and drugs and alcohol do not appear to have played any part in his death.

Thursday, July 19, 2012

FOMU ZINAENDELEA KUTOLEWA KWA MUHULA MPYA!

Zikiwa zimesalia siku chache hadi kufikia mwishoni mwa mwezi huu wa saba ambapo usajili rasmi wa wanafunzi wapya kujiunga na chuo utafungwa, chuo chetu cha TANZANIA E. COLLEGE kinawakaribisha wanafunzi wa siha zote kuja kujiunga ili kurahisishiwa suala la ajira kama muhula na kaulimbiu yetu isemavyo, SULUHISHO LA AJIRA, fomu zimeshaanza kutolewa kwa bei punguzo ya shilingi elfu kumi ambapo kwa hiyo hiyo elfu kumi utapatiwa kitambulisho cha chuo, usajili kamili, mafunzo ya kompyuta na vitendo, mawasiliano na pia uanachama wa chuo kamili, ufaulu huzingatiwa hapa chuoni ingawa kipaji ndio kitu kikuu ambacho chuo huangalia katika udahili wa wanafunzi wapya, ada hutofautiana kulingana na kozi ambayo mwanafunzi husika anaisoma, kwa jinsi mpangilio wa chuo ulivyo kwa muhula huu ni kwamba, itapofikia mwezi Agosti kutakuwa na ziara KUBWA ya kimafunzo kuelekea bagamoyo na pia katika ziara hiyo kutakuwa na kuhudumiwa kwa kila kitu na chuo ila tu mwanafunzi atachangia kidogo, tunawakaribisha wote kwa ajili ya kubadilisha mlolongo wa maisha yenu.
IMETOLEWA NA MKUU WA CHUO,
TANZANIA E. COLLEGE.

Wednesday, July 18, 2012

MUNGU AKUPE MOYO WA SUBRA BI. Mwantum Mbilikira

BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA, JINA LA BWANA LIHIMIDIWE,
INNALILLAH LA INNALLILAHI LAAJUN.
Tunawapa pole wale wote walioguswa na msiba wa mtoto wa Staff mwenzetu bi. Mwantum Rashid Mbilikira, ilikuwa ni siku ya majonzi kwa wote waliohudhuria msiba ambapo majira ya saa moja usiku siku ya jumatatu tarehe 16 Julai 2012 kilitokea kifo hicho cha malaika mdogo huyo ambaye hatutaacha kumkumbuka kwa makeke yake, raha zake na pia ucheshi wake na hasa hata kama mzazi amerudi na stress yaani msongo, malaika huyo kwa uwezo wake alikuwa anazitoa kwa namna ya kipekee na wazazi wake wamekiri na ni mashahidi wa jambo hili, chou chote cha TANZANIA E. COLLEGE kinaungana na familia nzima kuanzia hatua ya kwanza hadi ya mwisho katika wakati mgumu huu na wa majonzi kwa staff mwenzetu, tunaomba mwenyezi mungu ampe roho ya subra na ambariki liweze kumpita hili jambo mawazoni mwake maana hawezi kushindana na kudra pia matakwa ya mwenyezi mungu, mungu ndiye mtoaji na sisi tuko nyuma yake, mwenyezi mungu ambariki ustaadh Rashid pia naye ampe subra kama kwa mkewe vivyo hivyo, tunazidi kuwaombea na tunakumiss ofisini madam Mwantum, 
tu pamoja nawe!!
STAFF, TANZANIA E. COLLEGE.

Friday, July 13, 2012

WANAFUNZI TANZANIA E. COLLEGE WARIPOTI FIELD TENA

Wanafunzi wengine tena wa kozi ya Hotel Management wameripoti field katika hoteli ya MBEZI GARDEN maeneo ya Mbezi Beach jijini Dar es salaam, wanafunzi hao ni bi. Sauda Kika na Bw. Felson Mpenela, wakati Ndg. Elias Rashid yeye ameripoti kwa field pia jijini Tanga katika hoteli ya NYUMBANI, chuo kinawatakia mafanikio mema na wamalize salama mafunzo yao.

ELIMU KWANZA, UNAMKUMBUKA MWANAFUNZI HUYU?

Unakumbuka February 8 2012 wakati baraza la mitihani lilipotangaza matokeo ya kidato cha nne? stori kubwa ilikua mwanafunzi alieamua kuandika mistari ya bongo fleva kwenye sehemu ya kujibia maswali.
“nashukuru sana wanaosahihisha mitihani hii ya shule yangu, nitakapofeli naendelea na fani yangu ya bongofleva, Majita wangu wako levo za juu  na sio East Zuu, kukosa ni kawaida kwa binadamu” hiyo ilikua ni swali namba 6 na 7
kwenye swali la 11 kwenye moja ya mitihani yake aliandika mistari ya bongofleva kwamba “acha utani my girl, unakuja nyumbani umezizi mwenzako huku naona sijiwezi, kazi hiyo ya kuzizi nakwambia ukweli mwanzo ulikua mzuri lakini mwisho ukawa mbaya”
Baada ya hayo matokeo watu wengi ana walitamani kumfahamu huyu mwanafunzi, Jina lake la kuzaliwa ni Julius lakini la kisanii ni Elinaja, na ametoa sababu 5 za kwa nini aliamua kuandika hiyo mistari ya bongo fleva kwenye mitihani yake ya kumaliza kidato cha nne.
Amesema “1 ni kutaka kutuma ujumbe kwa watu wanaosimamia Elimu kwa ujumla, sababu ya pili ni kutaka kusaidia watu wanaoteseka mtaani ambao wanaishi maisha magumu kwa sababu tu ya kushindwa kwendana na system ya elimu iliyopo ambayo ukishindwa kwenda nayo sawa umefeli, tulivyoumbwa kuna mtu anaweza akawa anashindwa kitu flani lakini ni mzuri kwenye kitu kingine sasa mfumo uliopo hautoi nafasi kwa wasioweza hiyo system, sababu ya tatu ni kutokana na utaratibu wa usaishaji wa mitihani kwa sababu sijui kama kuna mwanafunzi yeyote aliewahi kufanya mtihani wake wa mwisho alafu mtihani wake ukarudishwa ili kuona wapi alipokosa na wapi alipopata”
“Sababu ya nne ni kuhusu wazazi kutambua uwezo wa watoto wao toka wakiwa wadogo kipi wanaweza kipi hawawezi ili kuokoa muda na pesa, sababu ya tano ni kwa serikali ijaribu kuweka shule za vipaji toka mwanafunzi akiwa mdogo kabisa, leo hii kuna mtu amepata degree pale chuo kikuu kasoma miaka mitatu na kupewa degree ya sanaa lakini hawezi kukuonyesha cheti hata kimoja kwamba alikua na elimu ya awali ya hiyo degree, huwezi kuniambia una degree wakati hukupata elimu ya msingi ya ulichosomea”
“Kwa namna moja au nyingine sidhani kama nimefanikiwa kwa sababu nilichofanya watu walikichukulia tofauti sikufanikiwa ndio maana nimeamua kujitokeza kumalizia kazi ambayo niliianza kuifanya kule kwa sababu nafsi yangu ilikua inanisuta, ila kwa sasa watu watakua wameelewa na ninaweza kuwasaidia watu wengine” – Julius (Elinaja)

Tuesday, July 10, 2012

HII NDIO TSHIRT YA CHUO CHETU.

Kwa bei ya shilingi elfu kumi tu unapata mng'aro huo hapo juu ambao ni lazima uvaliwe kwa siku za jumatano na ijumaa hapa chuoni, kuanzia utengenezaji wake hata kitambaa ni kiwango cha juu sana ambacho hata wanafunzi waliotangulia kuwa nazo wamesifia kuwa hakuna kama hizi kwa jiji hili, pata nawe yako moja ungare na wenzako!

Huu ni muonekano wa Mng'aro wa nyuma wa tshirt zetu za chuo, inapendeza ukiwa ndani yake, ni kitambaa kinachohimili na pia kitambaa chake maalum kwa ajili ya kukabiliana na hali za hewa mbili, twamaanisha joto na baridi, jionee mwenyewe.

USAJILI WA WANAFUNZI WAPYA BADO UNAENDELEA

Zikiwa zimesalia siku chache hadi kufikia mwishoni mwa mwezi huu wa saba ambapo usajili rasmi wa wanafunzi wapya kujiunga na chuo utafungwa, chuo chetu cha TANZANIA E. COLLEGE kinawakaribisha wanafunzi wa siha zote kuja kujiunga ili kurahisishiwa suala la ajira kama muhula na kaulimbiu yetu isemavyo, SULUHISHO LA AJIRA, fomu zimeshaanza kutolewa kwa bei punguzo ya shilingi elfu kumi ambapo kwa hiyo hiyo elfu kumi utapatiwa kitambulisho cha chuo, usajili kamili, mafunzo ya kompyuta na vitendo, mawasiliano na pia uanachama wa chuo kamili, ufaulu huzingatiwa hapa chuoni ingawa kipaji ndio kitu kikuu ambacho chuo huangalia katika udahili wa wanafunzi wapya, ada hutofautiana kulingana na kozi ambayo mwanafunzi husika anaisoma, kwa jinsi mpangilio wa chuo ulivyo kwa muhula huu ni kwamba, itapofikia mwezi Agosti kutakuwa na ziara KUBWA ya kimafunzo kuelekea bagamoyo na pia katika ziara hiyo kutakuwa na kuhudumiwa kwa kila kitu na chuo ila tu mwanafunzi atachangia kidogo, tunawakaribisha wote kwa ajili ya kubadilisha mlolongo wa maisha yenu.
IMETOLEWA NA MKUU WA CHUO,
TANZANIA E. COLLEGE.

Monday, July 9, 2012

Tumeiiba kidogo hii ili wadau wa blog yetu mpate kaburudani toka kwa kijana mwenzetu.


Je ikitokea bongo hii si tutapaogopa hata bungeni?


Baada ya kuzidiwa na maswali kwenye kipindi cha televisheni LIVE, mbunge wa bunge la Jordan kwanza alivua kiatu na kumtandika mpinzani wake kabla ya kutoa bastola yake na kutishia kumpiga risasi jamaa aliyekuwa akimbana sana kwa maswali. Mbunge wa bunge la nchini Jordan alishindwa
 kuvumilia maswali ya mpinzani wake na
 kuamua kutoa bunduki kwenye kipindi
 cha televisheni kilichokuwa kikirushwa LIVE
 na televisheni ya Jordan.

Mbunge huyo aliyetajwa kwa jina la 

Mohammed Shawabka alikuwa kwenye
 kipindi cha mjadala wa mambo ya
 kisiasa kilichokuwa kikirushwa 
LIVE na televisheni ya Jordan.

Mjadala huo ulipamba moto pale mbunge 

huyo alipotupiwa maneno na mwanaharakati 
 wa masuala ya kisiasa, Mansour 
Sayf al-Din Murad akituhumiwa kuchakachua
 uchumi wa Jordan huku mbunge huyo pia
 akimtuhumu mwanaharakati huyo
 kuwa ni jasusi wa Israel.

Mbunge huyo baada ya kuzidiwa na maswali 

ya mwanaharakati huyo alianza 
kumrushia maneno makali.

ASHA ROSE MIGIRO ATOA WARAKA MZITO

ALIYEKUWA Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Dk Asha-Rose Migiro ambaye anarejea nchini leo ametoa waraka maalumu akisema mwisho wa utumishi wake katika umoja huo ni mwanzo utekelezaji wa majukumu mengine hapa nchini.
Kauli ya Dk Migiro imekuja kipindi ambacho jina lake limekuwa likitajwa katika nafasi ya kumrithi Rais Jakaya Kikwete atakapomaliza muda wake wa kuongoza taifa mwaka 2015. Kabla ya kwenda UN, Dk Migiro alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Dk Migiro ambaye aliteuliwa na Katibu Mkuu wa UN, Ban Ki-Moon kushika mwaka 2007 wadhifa huo, alisema anafurahi kumaliza miaka mitano kwa mafanikio.
Katika waraka huo ambao gazeti hili limeuona jana, Dk Migiro alisema: “Hakika, kila chenye mwanzo hakikosi mwisho na kila mwisho wa jambo moja huwa mwanzo wa jingine.”
Alisema ingawa ni mapema kwake kutoa tathmini halisi ya utendaji wake kazi, wadhifa huo katika Umoja wa Mataifa umempatia uzoefu mkubwa.
“Kukitumikia chombo hiki cha kimataifa kwa muda wa miaka mitano na nusu mfululizo ni heshima ya pekee ambayo daima nitaienzi  kama kilele kimojawapo  cha mafanikio katika maisha yangu ya utumishi  wa umma. Kila siku niliyoitumia katika Umoja huo ilikuwa ni darasa la kusukuma mbele mipaka ya ujuzi na elimu,” alisema Dk Migiro.
Alisema amefahamu mambo mengi kuhusu umoja huo, dunia na watu wake ikiwamo ukomo  wa umoja huo katika kushughulikia matatizo mbalimbali yanayoikabili dunia.
“Daima nitaendelea kushukuru na kuthamini kwa dhati jinsi Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Serikali na Watanzania wenzangu walivyonitia moyo na kunienzi katika kipindi chote nilichokuwa Umoja wa Mataifa,” alisema.
Dk Migiro alisema utumishi wake katika umoja huo ulikuwa fursa adhimu iliyompa uzoefu wa kipekee hasa ikizingatiwa kwamba aliingia wakati ukikabiliwa na changamoto kubwa zikiwamo za maradhi, umaskini wa kupindukia na vitendo vya kikatili na udhalilishaji wa wanawake na watoto.
Alisema matatizo hayo na mengine yalimpa fursa ya kuchangia kikamilifu jinsi ya kukabiliana nayo wakati akitekeleza majukumu yake.
Dk Migiro alisema umoja huo umemwezesha kufahamiana na viongozi wengi wa kimataifa na watu mbalimbali wenye mafanikio duniani.... “Nimeweza kufahamu kwa undani thamani ya michango yao katika kujenga amani na ustawi wa dunia."
Alisema ingawa muda wake wa utumishi umekwisha kwenye umoja huo, ataendelea kuunga mkono jitihada za UN za kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoikabili dunia.
Sitasahau
Akizungumzia mambo aliyowahi kukutana nao katika utumishi wake, Dk Migiro alisema hatasahau hisia alizozipata kila alipokutana na watu wanyonge waliokuwa wanahitaji msaada wa Umoja wa Mataifa.
“Nitakumbuka daima tabasamu la mwanamke mmoja niliyekutana naye katika moja ya ziara zangu barani Afrika nilipotembelea zahanati mojawapo kati ya kadhaa zinazofadhiliwa na Umoja wa Mataifa,” alisema na kuongeza:
“Mama huyo mwenye watoto sita, alikuwa amekikumbatia kitoto chake kimoja kilichokuwa na afya dhaifu kwa kuumwa lakini alikuwa na tabasamu iliyojaa faraja na matumaini kwa kuwa alikuwa amefanikiwa kupata bure dawa za kunusuru maisha ya mwanawe.”
Alisema mama huyo pamoja na matatizo aliyonayo ya kuuguliwa na mwanaye, alipata faraja baada ya kuwa na uhakika wa kupata matibabu kwenye zahanati hiyo ya UN.
Dk Migiro alisema katika utekelezaji wa majukumu mengine, nguvu nyingi zilielekezwa katika kufanikisha Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs) na mengine yaliyokubaliwa kimataifa.
“Nilihamasika sana na dhamira waliyoionyesha wadau na washirika wetu wa maendeleo, zikiwemo Serikali, mashirika ya kiraia na mashirika ya biashara katika kufikia malengo ya milenia,” alisema.
Alisema anamaliza kipindi chake kukiwa na maendeleo mazuri yanayotokana na jitihada za kimataifa za kupambana na umaskini akisema mikakati ya UN ya kutaka kupunguza idadi ya watu maskini duniani kufikia angalau nusu ya viwango vya sasa, zimeanza kuzaa matunda.
“Taarifa hii ni ya kutia moyo licha ya ukweli kwamba dunia inapitia matatizo makubwa ya kiuchumi kuliko wakati mwingine wowote uliowahi kutokea katika miaka ya hivi karibuni,” alisema Dk Migiro katika waraka wake.
Dk Migiro alisema wakati wa utumishi wake katika umoja huo, ametumia nguvu kubwa na hadhi ya ofisi yake katika kupaza sauti za wanawake na wasichana ili kuleta usawa wa kijinsia.
“Tumeendesha kampeni za kupiga vita ukatili kwa wanawake na wasichana. Tumezihimiza mamlaka katika ngazi za kitaifa na kimataifa kutunga sera na sheria zinazozingatia haki za wanawake na usawa wa kijinsia na tumetaka wapewe fursa kushika nafasi za uongozi katika jamii,” alisema.
Alisema ili kufanikisha hilo, umoja huo ulifikia uamuzi wa kuanzisha idara ya umoja wa mataifa kwa madhumuni ya kuongoza masuala ya wanawake na masuala ya kijinsia.
“Tumefanya jitihada hizi kwa kuamini kuwa hakuna uamuzi wowote ule, uwe mdogo au mkubwa, unaofanywa na Umoja wa Mataifa bila ya kuzingatia maendeleo na ustawi wa wanawake na wasichana,” alisema.
Alisema katika eneo la afya ambako wanawake na watoto ndiyo wanaathirika wakubwa, juhudi zinafanywa kupunguza vifo na kuhakikisha kwamba kila mwanamke na mtoto anakingwa na maradhi ikiwamo kuzuia maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Alisema mwaka 2011, akiwa katika ziara jijini Nairobi, Kenya na Katibu Mkuu, Ban Ki-Moon  walipata fursa ya kukutana na mwanamke aliyeathirika na Virusi vya Ukimwi ambaye alijifungua watoto pacha watatu waliozaliwa bila ya kuambukizwa.
Tulifurahishwa na mpango wa kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto yanayosimamiwa na Umoja wa Mataifa,” alisema Dk Migiro.
Alisema umoja huo umekuwa ni mtetezi wa wanyonge na wenye kutaabika sehemu zote duniani na kwamba watumishi wake wanafanya kazi katika mazingira hatarishi kwa sababu hivi sasa bendera ya bluu si kinga tena akisema baadhi yao  wamekuwa wakiuawa katika matukio mbalimbali.
“Bendera ya buu haituhakikishii usalama kwani wengi wa watumishi wetu mahiri wamekuwa waathirika wa matukio ya kikatili ya ugaidi. Nilishuhudia tukio la aina hii huko Abuja, Nigeria ambako watumishi wenzetu walipoteza maisha kutokana na shambulio la kigaidi la Agosti 26, 2011,” alisema.
Alisema mara nyingi watumishi wa umoja huo wanapopoteza maisha, familia zao zinaachwa katika hali ngumu na kwamba kabla hajamaliza muda wake alianzisha mchakato wa kubaini namna bora ya kuwasaidia waathirika wa majanga hayo pamoja na familia zao

Friday, July 6, 2012

Si ndoto za Alinacha kweli hizi?

Lengo la serikali sio baya kama tuonavyo, sisi wanafunzi wa hapa kwa uchunguzi wetu tunahisi hili litakuwa suluhisho la foleni lakini hizi barabara za juu kweli kwa gharama hizo tulizoambiwa itawezekana kweli??
Kwa maneno mengine ni kuwa eti kinachofanywa hapo juu ni maandalizi ya muonekano kama huu, sisi ni wanafunzi tu wa chuo, labda kama kuna anayejua atuongezee ufahamu wa hili, picha ya juu ni maeneo ya manzese darajani ambapo ujenzi unaendelea ila hii ndo muonekano wa baadaye kwa sehemu zenye foleni kwa Dar.

Wanafunzi TANZANIA E. COLLEGE tunajiuliza....

  • Ni wapi vyombo vya habari vilipaswa kusimamia, kwa swala hili la kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa mgogoro kati ya serikali na Madaktari . Vyombo vya habari vinapaswa kuwaelimisha wananchi ni namna gani ya kujua nini haswa ni muhimu kwao, badala ya kujikuta wakiingia katika mabishano na mamlumbano yanayoashiria  kufurahia “Ubabe” wa wanasiasa vs madaktari.
  • Kwa sababu  bila wananchi kuwapa pressure hawa, wao (serikali na madaktari) wataendelea tu na huo mgogoro kwa gharama yetu – yaani sisi wenyewe tunaowashabikia (ama kwa kuchochea madaktari, au kwa kuchochea serikali).
  • Nina pata wasi wasi kidogo kwamba Magazeti, na watu wengi kwenye mitandao “social networks”, yakitokea matatizo, wanakua sehemu ya tatizo kwa kuongeza mafuta kwenye moto kwa mijadala ambayo mingine haina maana. KWASABABU KATIKA HILI, HAIJALSHI UKO UPANDE GANI, WOTE TUTAUMIA.
  • Hata tukisema wafukuzwe, au tukisema waendelee kugoma, TUTAUMIA TU!
  • La muhimu ni kuzibana pande zote mbili yaani serikali na Madaktari watueleze vizuri kwa nini wameendelea kung’ang’ania yao binafsi bila ya kuufikiria sisi na je ni kweli huwa wanatufikiria sisi....... sio tu kusema wako tayari kwa majadiliano kama vile suala hili halina uhitaji na umuhimu  na wa haraka.
  • Kwani  Vyombo vya habari,  vilipaswa  visiishie tu kuripoti tu: “serikali imesema wameshindwa kuafikiana…” au “madaktari wamesema wameshindwa kuafikiana…” Ilibidi vyombo vya habari viendelee kudadisi ili kukosoa kauli zao wote, na kwa kufanya hivo yawezekana vyombo vya habari vingekuwa wa kupeleka kwenye suluhu au makubaliano ya kudumu ya mgongano huo.
  • Unajua haitoshi tu kuripoti kuwa  serikali au madaktari wamesema wako tayari kwa majadiliano, bila kuwauliza haswa ni hatua gani wanafanya kuhakikisha majadiliano yanakuwapo.Na isiishie hapo tu, pia tuangalie ni nini kitakachofuata pale mgogoro utakapoisha…!
  • Upande mwingne tujiulize tunashughulika  vipi na viongozi ambao wamekua ni wabadhilifu katika matumizi kwenye sekta ya afya? Tunawabaini vipi madaktari walioshiriki katika wizi au upotevu wa kizembe wa madawa au vifaa vya hospitali?
  • Halafu na sisi wananchi wengine tujiulize je,  ….Hakuna miongoni mwetu tuliouza vifaa vibovu hospitalini na leo tunawalaumu wanasiasa au madaktari?
  • Lakini vipi ukiangalia kwa jicho la pili: “kiuchokozi”: Hivi wanasiasa wanaotupiana mpira katika hili suala, mara CCM, mara CHADEMA nakadhalika… kwa sasa wanatibiwa wapi? Ni jambo lisilo na kificho kuwa, idadi kubwa ya hawa wanasiasa ( bila kujali vyama vyao) wana “madaktari wao maalum/binafsi” au “vituo maalum” kwa ajili ya kuangalia afya zao na familia zao.
  • Kwa upande mwigine , ndugu zetu, rafiki zetu  madaktari - ni wangapi wana wateja maalum ambao ni wanasiasa hao hao waliovuruga mifumo katika sekta ya afya? Je, wanagoma kuwatibia hawa wakienda katika clinics zao binafsi? Hawa huitwa “Special clients” ambao ni hao hao viongozi, ambao leo wanawatuhumu ni chanzo cha huduma mbovu?
  • Ni wazi kuwa Vyombo vya habari  havijalichukulia swala hili kwa uzito unaostahili  na kulifanyia kazi ndani nje nje ndani na matokeo yake, sisi wananchi, baadhi yetu, tumeamua kubandika lawama au kutetea upande mmoja kati ya pande hizi mbili, bila kujua kwa kufanya hivyo, TUNAJIUMIZA WENYEWE!

Thursday, July 5, 2012

HIVI HAWA NDUGU MHHHHH.......

Lakini jamani kweli hivi ni ubunifu au mitindo ya kichuo chuo, lakini wazazi nyumbani taarifa hizi wanazo, haya siye kazi kuzitupia tu baaaaaaassss./......... hayo mengine yao.

MSAADA WA MAULIZO

Ebu tusaidiane kumuuliza huyu mjukuu wa ......................, amekuja chuoni kusoma au kukamata hawa wadudu wa chuoni? Hivi wazazi wake wanajua hii taaluma nyingine aliyojivisha kweli? Namba yake ni 06549485........ aaaaa hizo nyingine zilizobakia oteeni tu mumpigie maana hii balaa eti au???????

FULL KUSIKILIZA....

Ebu kaone kale kenye ribbon kichwani kwa paleeeee, halafu mkitoka hapo mnalalamika elimu Tanzania inashuka, kwa staili hiyo kweli????

Teacher JOS naye duh...

Teacher Joseph Lino katika pozi la picha hili, yaani ful kuambiwa ajiandae halafu 1, 2, 3 chhhhhhhhhhhhhhh

Julieth Julius naye hakuwa nyuma bwana....

Julieth Julius mamaaaa Kithethe jamani alikandamiza ipasavyo katika outdoor studio ya Tanzania E. College hiyo siku na kipindi chake cha maliasili.........

Sasa huyu naye, Miriam weee???

Yaani kama kalazimishwa vile, kwani ameambiwa kuwa akisomea kozi ya ualimu wa chekechea ndo awe hivi? Lazima kadanganywa na mtu, ndio poziiii au ni ghafla kashtushwa na flash???

SAUTI BYEGO TENA......

Tunasikiaga eti huwa anapenda tu kupiga picha hata kama hazina sababu, sasa hapa ndo nini?
Outdoor studio hiyo, chezea???

KWANI KUSOMA TU KWETU UNAFIKIRI?????

Yaani hizi picha ni za zamaaaaaaaaaaanii tulikuwa twapiga hivi, nimeona si vibaya niwadakishe wadau wa TANZANIA E. COLLEGE kiduchu mwone na vipaji vingine, sasa hiki ni kipaji gani sijui??? Eti "Rick..."

DANNY MAKALA NAYE HAKUWA NYUMA

Huyu ndiye Daniel Makala bwana, anawaonesha vijana wenzake wa Tanzania E. College kuwa hata huku nako yumo katika kutangaza na sio kule tu, yaani hapa kipindi cha michezoni wiki hii lazima kiende sawa, ni pale pale katika outdoor studio, TEC imejazana bwana mavipaji......

Mwajabu akikandamiza kwenye outdoor studio...

Huyu ndo bibie mwajabu aliyekuwa akishangaliwa na rais wa serikali ya chuo cha Royal Copllege of Tanzania, yaani ni hatari huyu ndugu kwa taarifa za habari, kwanini rais asishangae?

RAIS WA SERIKALI YA ROYAL COLLEGE ndani ya TANZANIA E. COLLEGE...

Huyu ni rais wa serikali ya wanafunzi wa Royal College of Tanzania chini ya Mzazi Chami, cha ajabu alikuwa akishangaa jinsi watoto wa Tanzania E. College walivyokuwa wakikamua ndani ya outdoor studio, kazoea kujifungia ndio maana kila kitu aliona kipya.........

Tuesday, July 3, 2012

HUYU MTOTO NA WATU WA CHADEMA JAMANI

Huyu mtoto ameanza mapema haya mambo, ni mwanafunzi tu huyu aliyemaliza mafunzo ya utangazaji hapa Tanzania E. College na sasa yuko hukooooooo Songea chanali moja laitwa Jogoo FM, ameshaingia kwenye siasa sijui maana huwa wanaanzaga hivi hivi, ni haka keupe keupe kidogo kapo na KATIBU UENEZI MKOA WA RUVUMA CHADEMA, ona kanavyojiamini eti, inabidi tupate undani je kulikuwa na biashara gani hapa, ukitaka kupata ukweli we mrukie hewani kwa namba 0654898001, mwenyewe ataongea.

MAMAA MIPASHO, HAPANA CHEZEA WEWEE.......

Hakuna asiyejua kuhusu huyu mtu hapa Tanzania E. College, ndiye mchaga wa kwanza kutangaza taarab kwa Afrika Mashariki hii, ukitaka umpate msikize kwenye 93.2 FM na kipindi cha mcharuko wa Pwani, kila jumamosi jamani, unamtaka huyu?

HIZI SIJUI NI MBWEMBWE AU............

Unakaona hako kasmall dady kwa nyuma pale, vituko darasani hadi nje ya darasa, ndio Josephat Basil huyo......

HUYU NDIYE NYAMARASA MGAYA



Sasa sijui hizi ni pozi au ni mikao ya kwetu kule kanda ya ziwa au kaskazini, eti naye ni Mwanafunzi wa Tanzania E. College na Kimara, unajua nini........?

VICHWA VYA TANZANIA E. COLLEGE

Mmoja wa wanafunzi wa Tanzania E. College Bw. Sauti Byego akiwa studio za chuo hiki akikandamiza maujuzi ya sauti, ila sio sauti jina lake, twamaanisha "voice", wanafunzi wa chuo hiki hufanya mazoezi kwa vitendo na hii ni jadi yetu.

Sunday, July 1, 2012

Serikali Kuleta Madaktari Kutoka Nje Ya Nchi - Bilioni 200 Zatengwa Kuwalipa-mbona sielewi hii filamu hivi muongozaji na mtunzi ni nani au ni ya kanumba?.





Serikali imeamua kuagiza madaktari kutoka nchi za nje watakaochukua nafasi ya wale wa hapa nchini ambao wamegoma kuanzia mwishoni mwa wiki iliyopita.

Habari kutoka katika moja ya vyanzo vya kuaminika zimesema kuwa uamuzi huo wa serikali ulipitishwa katika kikao cha Baraza la Mawaziri kilichokutana mjini Dodoma juzi chini ya uenyekiti wa Rais Jakaya Kikwete.

Habari kutoka ndani ya kikao hicho zilidai kuwa Rais Kikwete alikerwa na tabia ya madaktari kupingana na serikali licha ya juhudi zote zilizofanywa kuboresha maslahi yao.

Kwa mujibu wa habari hizo, kiasi cha sh bilioni 200 kimetengwa kwa ajili ya kuwaleta na kuwagharimia madaktari hao wa nje na pia baraza limepitisha azimio la kuzungumza na hospitali za jeshi kama Lugalo na zingine ndogo kubeba jukumu hilo kwa sasa pamoja kuagiza madaktari wastaafu wote warejee kazini katika kipindi hiki cha mgomo.

Habari zimedai kuwa madaktari hao wanasadikiwa watatoka katika nchi rafiki, zikiwemo India, China, Cuba na Afrika Kusini, na kwamba wataziba kikamilifu pengo la wale wa hapa nchini ambao wamegoma.

Inaelezwa kuwa mara baada aya kukamilika na kuanza rasmi kwa huduma za matibabu, madaktari wa hapa nchini waliomo katika mgomo na wale zaidi ya 200 waliodaiwa kufukuzwa na serikali kimyakimya, watalazimika kurejeshwa kazini kwa masharti makali.

Hata hivyo, uamuzi wa serikali kuwatimua madaktari wakati suala lao liko mahakamani, umewagawa wabunge.

Baadhi ya wabunge walijaribu kuhoji suala hilo Bungeni, lakini walikwama baada ya Spika Anna Makinda kuzuia mjadala huo kwa madai kuwa suala hilo liko mahakamani.

Mbunge wa Nzega, Dkt. Hamis Kigwangala, alisema kuwa kilichofanywa na serikali ni kiini macho kwani juzi Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisema serikali haiwezi kutoa kauli dhidi ya madaktari kwa madai kuwa kuna kesi mahakamani, “Juzi serikali imesema kuwa haiwezi kutoa kauli kwa vile jambo hilo lipo mahakamani, sasa imewezaje kuwafukuza madaktari wakati jambo lipo mahakamani?” alihoji Dkt. Kigwangala.

Aliitaka serikali kuondoa kesi hiyo ili kurejesha majadiliano kwani ndio njia pekee ya kukabiliana na mgogoro huo.

Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, alimshangaa Spika Anna Makinda kuzuia mjadala huo kwani ungeweza kujadiliwa bila kuingilia uhuru wa mahakama.

Juzi uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, uliwafukuza kazi madaktari 229 walioko katika mafunzo kwa njia ya vitendo kutokana na mgomo unaoendelea wa kushinikiza kulipwa posho zao za mwezi mmoja.

Hospitali zingine ambako madaktari wamefukuzwa kutokana na mgomo huo ni pamoja na Mbeya na Dodoma. Tafakari hili !!!!
 
 Na Fadhili Athumani
 

HOTUBA YA MHE. DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, KWA WANANCHI, TAREHE 30 JUNI, 2012


Ndugu Wananchi,
              Kama ilivyo ada naomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehma, kwa kutujaalia uzima na kutuwezesha kumaliza nusu ya kwanza ya mwaka 2012 salama.  Kwa kutumia utaratibu wetu wa kuzungumza nanyi kila mwisho wa mwezi, leo napenda kuzungumzia mambo mawili. Jambo la kwanza ni suala la usafirishaji haramu wa binadamu nchini na la pili ni la mgomo wa madaktari. 
Usafirishaji Haramu wa Binadamu Nchini
Ndugu Wananchi;
              Bila ya shaka mtakuwa mmezisikia taarifa za tukio la kushtusha na kuhuzunisha la kukutwa maiti 43 za watu wasiojulikana, zilizotupwa katika kichaka kilichopo kijiji cha Chitego, Wilayani Kongwa, Mkoa wa Dodoma tarehe 26 Juni, 2012.  Pamoja na maiti hao, walipatikana watu 84 wakiwa hai lakini wote wakiwa wamedhoofu na baadhi yao wakiwa mahututi.  Hatua za haraka zilichukuliwa kuwasafirisha watu hao hadi Dodoma ambapo wale waliokuwa mahututi walifikishwa Hospitali Kuu ya Mkoa wa Dodoma kwa matibabu na wengine walihifadhiwa katika Kituo cha Kati cha Polisi, Dodoma.  Maiti 22 zilipelekwa Dodoma na 21 zilipelekwa Morogoro kuhifadhiwa.
Taarifa zilizopatikana kutoka kwa wale walionusurika zimebainisha kuwa watu hao ni raia wa Ethiopia ambao walikuwa safarini kwenda Malawi na baadaye Afrika ya Kusini ambako wangetengenezewa utaratibu wa kwenda kuishi Marekani na Ulaya.  Kwa mujibu wa maelezo yao, safari yao ilianza miezi mitano iliyopita.  Mwezi mmoja waliutumia Ethiopia na miezi minne waliitumia Kenya kabla ya kuletwa Arusha ambako walipakiwa kwenye lori na kuanza safari ya kuelekea Malawi lakini ikaishia Chitego.  Lori walilopanda lilikuwa limezibwa kabisa na hivyo kusababisha vifo kwa kukosa hewa.
Tukio la Chitego, Dodoma la wahamiaji haramu kukamatwa na wengine kukutwa wamekufa si la kwanza kutokea hapa nchini.  Kwa jumla, katika kipindi cha takriban miaka 10 sasa kumekuwepo na tatizo kubwa la wahamiaji haramu kuingia nchini.  Kwa mfano, kati ya mwaka 2005 na hivi sasa jumla ya wahamiaji haramu 19,683 wamekamatwa.  Karibu wote wameshaondoshwa nchini na hivi sasa wapo karibu watu 1,500 tu magerezani wanaotumikia adhabu na kusubiri kurejeshwa makwao.  Wengi wa watu hao wanatoka Ethiopia na Somalia na baadhi kutoka Pakistan na Bangladesh.
Wahamiaji haramu wamekuwa wanaingia nchini kwa kupitia njia zisizo rasmi.  Wapo wanaotumia nchi kavu hasa kupitia mikoa ya Mara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga.  Na, wapo wanaopitia baharini kwa kutumia fukwe za Pemba, Unguja na za mikoa ya ukanda wa Pwani ya Tanzania Bara yaani Tanga, Pwani, Lindi na Mtwara.
Ndugu Wananchi;
Kwa mujibu wa kauli zao, watu hao wamekuwa wanaeleza kuwa hawaji nchini kuhamia bali wao ni wapita njia tu.  Wanaelekea Afrika ya Kusini ambako wameahidiwa kuwa watatengenezewa mipango ya kuhamia Marekani na Ulaya.  Watu hao pia wamethibitisha kuwepo kwa watu maalum wanaojihusisha na usafiri wao tangu nchi watokako na zote wanazopitia mpaka kule waendako.  Aidha, wamesema kuwa wao wanawalipa watu hao ili wawasafirishe na hakika si kiwango kidogo.  Kwa jumla ni kwamba hili si suala la uhamiaji haramu bali ni la biashara haramu ya kusafirisha binadamu.
Ndugu Wananchi;
Kufuatia vyombo vyetu vya usalama kuwa makini na watu wengi kukamatwa ndipo wasafirishaji walipobuni njia za kuwasafirisha kama mizigo.  Makontena, malori yaliyofunikwa nyuma na matenki ya mafuta na ya maji yamekuwa yanatumika kwa ajili hiyo.  Usafiri wa aina hiyo ndiyo uliosababisha vifo vilivyotokea Dodoma tarehe 26 Juni, 2012 na vya watu 21 vilivyotokea mwezi Desemba, 2011 Mkoani Morogoro, na vile vya watu 12 vilivyotokea katika matukio mawili ya Mkoa wa Mbeya, mwezi Mei, 2012.
Ndugu Wananchi;

  

Tarehe 27 Juni, 2012 nilikutana na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama nchini kuzungumzia tukio la Chitego na suala zima la biashara hii haramu na hasa mbinu mpya inayotumiwa na wasafarishaji.  Nilitoa pongezi kwa vyombo vya dola kwa kazi nzuri waifanyayo kudhibiti shughuli za biashara hii haramu hapa nchini.  Tulielewana kuwa waendelee kuimarisha udhibiti huo kwa lengo la kukomesha kabisa biashara hii.
Niliagiza pia kwamba kikundi kazi nilichokiunda mwaka 2006 kushughulikia ujambazi sasa kielekeze sehemu ya nguvu zake kukabili tatizo hili. Aidha, kwa pamoja tulikubaliana kuwa nchi yetu ishirikiane na wenzetu wa Ethiopia, Kenya, Malawi, Msumbiji na Afrika ya Kusini kutambua mawakala na kuwabana kwa mujibu wa sheria.  Tayari nimeshaanza kufanya mawasiliano na baadhi ya Wakuu wa Nchi hizo kuhusu ushirikiano huo.  Nashukuru wote wameafiki nchi zetu zishirikiane kwa pamoja kuvunja mtandao huu mchafu na kutokomeza biashara hii haramu na inayodhalilisha utu wa mwanadamu.
Ndugu Wananchi;
Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wenzetu, wakazi wa vijiji vya Chitego na Mkoka kwa kazi nzuri walioifanya. Kwa kweli, wenzetu wameonesha uzalendo wa hali ya juu kwa kutoa taarifa mapema juu ya jambo lenyewe, lakini pia wameonesha utu kwa kuwajali wageni waliokumbwa na janga hili. Naushukuru pia uongozi wa Mkoa wa Dodoma na Morogoro ikiwa ni pamoja na vyombo vya ulinzi  na usalama kwa kulishughulikia tatizo hilo kwa umakini mkubwa.   Nimefurahishwa sana na ushirikiano ulioonyeshwa na vyombo na taasisi mbalimbali za Serikali katika kushughulikia suala hili.
Mgomo wa Madaktari
Ndugu Wananchi;
              Jambo la pili ni kuhusu mgomo wa Madaktari unaoendelea nchini hivi sasa.  Nilipozungumza na Wazee wa Dar es Salaam katika Ukumbi wa Diamond Jubilee tarehe 12 Machi, 2012, kuhusu mgomo wa Madaktari uliokuwa unaendelea wakati ule pamoja na kuelezea chimbuko la mgomo na hatua iliyokuwa imefikiwa, nilielezea mazungumzo yangu na viongozi wa Chama cha Madakari wakiwemo pia viongozi wa Jumuiya ya Madaktari.  Nilitoa taarifa kuwa tumeelewana kuwa watasitisha mgomo na watarudi kwenye meza ya majadiliano na Serikali.  Siku ile pia nilielezea matumaini yangu kuwa mgomo ule utakuwa wa mwisho katika nchi yetu.  Bahati mbaya matumaini yangu hayo hayakuwa na hivi sasa tunashuhudia tena wagonjwa wakiteseka, kuhangaika na wengine kufa kwa sababu ya kukosa huduma wanazostahili kwa vile madaktari wao wamegoma tena.
Ndugu Wananchi;
Kama walivyoniahidi, madaktari waliacha kugoma na viongozi wao walirudi kwenye mazungumzo na Serikali.  Kama ilivyoagizwa na Mahakama Kuu, Kitengo cha Kazi tarehe 8 Machi, 2012, kwa mujibu wa Sheria ya Mahusiano Kazini, Namba 6 ya mwaka 2004.   Chama cha Madaktari na Serikali walifika katika Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (Commission for Mediation and Arbitration) kwa ajili ya majadiliano.  Kwa pamoja na kwa ridhaa yao wote, pande hizo mbili ziliiomba Tume hiyo iwape fursa ya kuzungumza wao wenyewe na wakimaliza mazungumzo wataenda kusajili makubaliano yao.  Tume ikawakubalia.  Ni vizuri ikakumbukwa kuwa siku ile ya tarehe 8 Machi, 2012 Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi, ilitoa zuio la mgomo pamoja na kuagiza kuwepo mazungumzo baina ya pande mbili.
Ndugu Wananchi;
Kati ya tarehe 10 Aprili, 2012 na tarehe 30 Mei, 2012, vilifanyika vikao sita vya majadiliano kati ya Serikali na Chama cha Madaktari.  Katika mazungumzo hayo hoja au madai 12 ya madaktari yalizungumzwa.  Mambo hayo ni haya yafuatayo:
1.     Posho ya kuitwa kazini (on call allowance) iwe asilimia 10 ya mshahara.
2.     Posho ya kufanya kazi katika mazingira hatarishi (Risk allowance) iwe asilimia 30 ya mshahara.
3.     Madaktari wapatiwe nyumba grade A au posho ya makazi ambayo iwe asilimia 30 ya mshahara.
4.     Posho ya kufanya kazi katika mazingira magumu iwe asilimia 40 ya mshahara.
5.     Madaktari walipwe posho ya usafiri ya asilimia 10 ya mshahara au wakopeshwe magari.
6.     Madaktari wanaoanza kazi walipwe mshahara wa shilingi 3,500,00/= kwa mwezi.
7.     Madaktari wapatiwe Green Card za Bima ya afya.
8.     Hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi ya Watendaji Wakuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
9.     Viongozi wa Kisiasa kulazimisha kupewa rufaa nje.
10.            Madaktari waliofukuzwa warudishwe kazini.
11.            Huduma za afya ziboreshwe nchini.
12.            Posho ya uchunguzi wa maiti iongezwe.

Ndugu Wananchi;
              Katika mambo hayo 12 pande zote mbili zilifikia muafaka na kukubaliana wa pamoja kwa mambo saba.  La kwanza, ni kuhusu usafiri wa kwenda na kurudi kazini.  Serikali ilieleza kuwa upo utaratibu kwa mujibu wa Waraka wa Utumishi wa Serikali Na. 3 wa mwaka 2011 wa kuwakopesha wafanyakazi wa Serikali fedha za kununulia magari au pikipiki, samani na matengenezo ya magari.  Ilikubaliwa kuwa madaktari waitumie fursa hiyo.
              Jambo la pili, ni kuhusu madaktari kupatiwa Green Card za Bima ya Afya.  Jambo hili lilikubaliwa na Serikali na Wizara ya Afya imekwishachukua hatua za utekelezaji wake.
              Jambo la tatu, ni kuhusu hatua za kinidhamu kuchukuliwa dhidi ya Watendaji Wakuu wa Wizara ya Afya.  Kwa pamoja walikubaliana kuwa suala hilo liko nje ya mamlaka ya Kamati yao ya pamoja, waziachie mamlaka husika za uteuzi.  Uongozi wa juu wa Wizara umebadilishwa na sasa kuna uongozi mpya.  Lakini, jambo la kustaajanisha hata Waziri mpya wa Afya alipowataka waonane kuzungumzia hoja walikataa kumuona.  Kwanza walisema hawaoni sababu kwa vile wameyazungumza na Kamati yake kwa miezi mitatu bila ya mafanikio
              Jambo la nne walilokubaliana ni kuhusu viongozi kulazimisha kupewa rufaa ya kutibiwa nje.  Walikubaliana mambo mawili.  Kwanza, kwamba maelekezo ya Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda kuwa madaktari wazingatie maadili ya kazi zao na kukataa kutoa rufaa kwa mtu asiyestahili awe kiongozi au asiwe kiongozi. Pili, walikubaliana kuwa hospitali zilizopo ziboreshwe ili viongozi watibiwe hapa nchini.  Ukweli ni kwamba kufanya hivyo ndiyo sera ya Serikali.  Nililieleza hili mwezi Desemba 30, 2005 katika hotuba yangu ya kuzindua Bunge baada ya kuchaguliwa kwa mara ya kwanza kuongoza nchi yetu. 
Tumeiongeza sana bajeti ya sekta ya afya kutoka shilingi bilioni 300 2005/2006 hadi shilingi trilioni 1.2 mwaka 2011/12 na imekuwa ya tatu baada ya miundombinu na elimu.  Tumeziimarisha hospitali za Mikoa kwa vifaa tiba na wataalamu wa afya.  Kazi inaendelea katika hospitali za Wilaya. Tumewekeza katika Hospitali ya Muhimbili.  Hospitali hiyo ilivyo leo sivyo ilivyokuwa miaka sita nyuma.  Na kazi inaendelea hasa katika maeneo ambayo tunapeleka wagonjwa nje.  Matunda yake yanaanza kuonekana kwa upande wa figo, moyo, kinywa na mipango inaendelea kwa upande wa ubongo na mishipa ya fahamu.  Tunaendelea kuimarisha mafunzo ya  madaktari na madaktari bingwa, yote kwa nia hiyo hiyo.  Hivi sasa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba,Muhimbili kinachukua wanafunzi wengi zaidi ya ilivyokuwa siku za nyuma na makazi mapya ya chuo yanaendelea kuandaliwa ili kuchukua wanafunzi wengi zaid.    Mwaka 2005 tulikuwa na madaktari bingwa 46 mwaka huu tunao 520.
Ndugu Wananchi;
              Jambo la tano ambalo pande zote mbili zilikubaliana ni kuhusu madaktari waliofukuzwa.  Hawa ni wale Interns waliokuwa wamerudishwa Wizarani kutoka Muhimbili na kupangiwa hospitali za Temeke, Ilala, Mwananyamala na Lugalo.  Hili ni jambo ambalo lilikuwa limemalizika kitambo na wote walikuwa wamerudi Muhimbili.
              Jambo la sita ni kuhusu mapendekezo mbalimbali yaliyotolewa na madaktari kuhusu kuboresha huduma ya afya.  Mapendekezo hayo yalihusu kutathmini sera na mpango wa afya ya msingi, bajeti ya afya kuwa asilimia 15 ya bajeti ya Serikali, kuwepo na utaratibu mzuri wa kuajiri madaktari na kuboresha viwango vya ubora wa madaktari na kadhalika.  Serikali imeyaafiki mapendekezo hayo na yatafanyiwa kazi.
              Jambo la saba, ambalo pande zote walilokubaliana ni kuhusu kuongeza posho ya uchunguzi wa maiti.  Hili ni jambo jipya halikuwepo mwazoni.  Hata hivyo, Serikali imelikubali na posho hiyo imeongezwa kutoka shilingi 10,000/= hadi kufikia shilingi 100,000/= kwa daktari na shilingi 50,000/= kwa wasaidizi wake.
Ndugu Wananchi;
              Kuna masuala matatu ambayo yamekuwa na muafaka kwa kiasi fulani na kutoafikiana kwa baadhi ya mambo.  La kwanza ni suala la kufanya kazi katika mazingira hatarishi.  Serikali imekubali hoja ya kuchukua hatua ya kuwalinda madaktari wanaofanya kazi katika mazingira hatarishi.  Serikali iliwaeleza kuwa watumishi wa kada zote za afya watapatiwa chanjo dhidi ya maambukizi ya Hepatitis B na fedha zimetengwa katika bajeti ya 2012/13.
Aidha, Serikali imeeleza dhamira ya kurudisha posho ya mazingira hatarishi kwa watumishi wa umma wanaostahili.  Utekelezaji wake utafanyika baada ya uchambuzi wa kina wa kubainisha mazingira hatarishi ni yepi, viwango stahiki viwe vipi na nani hasa wahusike.  Madaktari wamekataa hili la kufanya uchambuzi, wanataka kiwango kiwe kama wanavyotaka wao, yaani asilimia 30 ya mshahara na kianze mara moja.
              Jambo la pili ambalo wamekubaliana nusu nusu ni kuhusu nyumba za kuishi.  Serikali imekiri wajibu wake wa kuwapatia madakari nyumba za kuishi.  Aidha, imeeleza mpango ulioanza wa kujenga nyumba 700 za madaktari kote nchini na kwamba hivi sasa ujenzi wa nyumba 90 unaendelea, 50 katika mkoa wa Mtwara na 40 katika mkoa wa Rukwa.
Kwa maeneo ambayo madaktari wanalipwa posho ya pango Serikali imesema waajiri wataendelea kufanya hivyo kwa mujibu wa taratibu zilizopo kwa watumishi wa umma wenye stahili ya kupewa nyumba.  Jambo hilo limekataliwa na Madakari na kutaka lazima walipwe asilimia 30 ya mshahara kama posho ya nyumba.  Serikali kwa upande wake imeona vigumu kufanya hivyo na kuwasihi wakubali wanayotendewa wafanyakazi wengine wote wa umma.
              Jambo lingine ambalo lilikuwa na makubaliano ya nusu nusu ni kuhusu posho ya kufanya kazi katika mazingira magumu.  Pande zote mbili ziliafikiana kuwa yapo baadhi ya maeneo nchini yanayo mazingira magumu kwa watumishi wa umma  hivyo hatua zichukuliwe kuwasaidia watumishi hao. Serikali imekubali wajibu wa kuweka utaratibu wa kuboresha maisha ya watumishi katika maeneo hayo.  Kwa ajili hiyo, Serikali itatoa mwongozo kwa mamlaka za ajira kuhusu namna ya kuwasaidia watumishi hao kupunguza makali ya maisha katika kila eneo badala ya kutegemea posho peke yake.
  Kuhusu posho, Serikali imeeleza kuafiki kuwepo posho ya aina hiyo ila itatekelezwa baada ya kufanya uchambuzi wa kuainisha mazingira husika, kutambua watumishi waliopo na gharama zake.
              Madaktari hawajakubali kusubiri zoezi la uchambuzi lifanyike, wanataka Serikali ilipe posho hiyo sasa.  Tofauti hapa si posho hiyo kuwepo, bali ni rai ya Serikali ya kubaini maeneo yenyewe na kupanga aina ya hatua na viwango vya posho kulingana na mazingira halisi ya maeneo.  Madaktari hawaoni haja ya kufanya hayo.
Ndugu Wananchi;
              Mambo mawili hayakuwa na muafaka kabisa kati ya pande zetu mbili.  Jambo la kwanza ni posho ya kuitwa kazini (on call allowance).  Kwanza sina budi kueleza kuwa Serikali imekubali kuongeza posho hiyo.  Tangu Februari, 2012 posho iliongezwa kutoka shilingi 10,000/= hadi shilingi 25,000/= kwa daktari bingwa (Specialist), shilingi 20,000/= kwa dakari mwenye usajili wa kudumu (Registrars) na shilingi 15,000/= kwa madaktari waliohitimu ambao wapo katika kipindi cha mafunzo kazini (Interns).  Viwango hivyo vya posho vinatumika hivi sasa. 
  Madaktari kwa upande wao hawakukubali uamuzi huo wa Serikali na kusisitiza walipwe asilimia 10 ya mshahara.  Ugumu wa kukubali pendekezo la madakari ni kuwa sharti la malipo haya ni mtu kuitwa kazini.  Ukitaka ilipwe kiwango cha mshahara ina maana kuwa hata kama daktari hakupangwa kuitwa au alipangwa na hakutokea aendelee kulipwa.  Hili haliwezi kuwa sahihi kufanya.  Linaweza kuwafanya baadhi ya madaktari kutokutimiza wajibu wao kwa vile wana hakika mwisho wa mwezi malipo yako pale pale.
Ndugu Wananchi;
Jambo la pili ambalo muafaka haukufikiwa baina ya Serikali na madaktari ni kuhusu mshahara wa kuanzia kazi wa daktari.  Madaktari wanataka uwe shilingi 3,500,000/= wakati Serikali inasema kiasi hicho hatukiwezi.  Serikali imeeleza utayari wake wa kuongeza mshahara kwa kati ya asilimia 15 mpaka 20 kama ambavyo itafanya kwa watumishi wote wa umma katika mwaka huu wa fedha.  Kwa kiwango cha sasa cha mshahara wao, daktari ataanzia kati ya shilingi 1,100,000/= na 1,200,000/= kutegemea kiwango kipi hatimaye kitaamuliwa.  Madaktari wamekataa katakata na wameng’ang’ania shilingi 3,500,000/=.
Ndugu Wananchi;
Huo ndiyo mlolongo wa mambo yaliyozungumzwa na pande zote mbili na matokeo ya mazungumzo yenyewe.  Katika kikao cha sita kilichofanyika tarehe 30 Mei, 2012, upande wa Chama cha Madaktari ulisema kuwa kwa vile hoja ya nyongeza ya mshahara haina mabadiliko hawakuona haja ya kuendelea na majadiliano mpaka watakapowasiliana na wenzao.  Waliahidi kutoa taarifa ndani ya wiki mbili.  Tarehe 12 Juni, 2012, Rais wa MAT aliandika barua kwa Katibu Mkuu Utumishi ambaye ndiye kiongozi wa majadiliano kwa upande wa Serikali, kuwa Madaktari wameikataa taarifa na ufafanuzi waliopewa kutoka Serikalini kwa ujumla wake.
Ndugu Wananchi;
Baada ya majibu yale ya madaktari, tarehe 19 Juni, 2012, Serikali na Madaktari walikwenda kwa Msuluhishi (CMA) kutoa taarifa kuwa mgogoro umekosa usuluhishi kama sheria inavyotaka.  Kwa pamoja pande zote mbili zilikubaliana suala hilo lifikishwe Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi.  Wakati pande zote zinasuburi mgogoro huu kufikishwa ngazi hiyo ya juu, upande wa Madaktari ukatangaza kuwepo kwa mgomo kuanzia saa sita ya usiku tarehe 23 Juni, 2012.  Hatua hiyo haikustahili kwani suala lenyewe halijafika mwisho wa kushughulikiwa kwa mujibu wa Sheria za Mahusiano ya Kazi nchini.
Ndugu Wananchi;
Tarehe 22 Juni, 2012, Mwanasheria Mkuu wa Serikali akaenda Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi kulifikisha suala la tishio la mgomo na kuomba zuio la muda kufanywa.  Mahakama Kuu ilikubali ombi hilo na kuagiza kuwa mgomo usitishwe.  Juhudi za kumtafuta Rais wa MAT, Dkt. Namala Mkopi na viongozi wengine wa MAT hazikufanikiwa, Ofisi ya MAT ilikuwa imefungwa na simu zote za viongozi wa MAT zilikuwa zimezimwa.  Hatimaye tarehe 25 Juni, 2012, alipatikana na kupewa amri hiyo ya Mahakama.  Tarehe 26 Juni, 2012, Dkt. Mkopi alifika Mahakamani ambapo alikana kuwa yeye hahusiki na kuitisha huo mgomo lakini hakumtaja aliyehusika.  Pamoja na rai hiyo, Jaji alimuamuru Rais wa MAT akawatangazie wanachama wake kusitisha mgomo.  Dkt. Namala Mkopi hajafanya hivyo hadi leo na mgomo umekuwa unaendelea kinyume cha Sheria.
Ndugu Wananchi;
Wagonjwa wanateseka na wengine kupoteza maisha kwa mgomo huu usiokuwa halali kisheria ambao pia haustahili kuwepo hata kwa mujibu wa maadili ya udaktari.  Viongozi wa MAT na wenzao wanawaingiza Madaktari katika mgogoro na Mahakama na waajiri wao isivyostahili.  Ni vyema viongozi wa Madaktari na madaktari wakatambua kuwa wanashiriki katika mgomo usiokuwa halali ambao pia kiongozi wao mkuu amekana Mahakamani kuwa hahusiki nao.  Madaktari lazima watambue pia kwamba ajira zao wanaziweka hatarini.  Mfanyakazi ana kinga ya kutofukuzwa kazi na mwajiri kwa kushiriki mgomo unaokubalika kisheria.  Huu siyo.  Watapoteza ajira, hawana pa kukimbilia, hawana cha kiwalinda.  Kwa madaktari interns, wanahatarisha maisha yao kwani hawatapata cheti cha kudumu wakishiriki mgomo usiokuwa halali.   Lazima watafakari sana kwa hayo wafanyayo. 
Ndugu Wananchi;
              Napenda kurudia maneno niliyoyasema tarehe 12 Machi, 2012, kuwa kuboresha mishahara na maslahi ya wafanyakazi ni Sera ya Serikali yetu kwa maelekezo ya Ilani ya Chama Tawala (CCM).  Tumeitekeleza kwa vitendo sera hiyo, hata hivyo ni ukweli ulio wazi kuwa nia yangu njema tu pekee haitoshi, lazima uwezo wa kufanya hivyo uwepo.  Kwa kulingana na uwezo uliopo, tumeendelea kuboresha mishahara na maslahi ya wafanyakazi hatua kwa hatua tangu tuingie madarakani.  Tumefanya hivyo kwa jumla kwa wafanyakazi wote na kwa kada mbalimbali za watumishi wa umma.
Miongoni mwa wafanyakazi wa umma walionufaika na hatua hizo za Serikali ni madaktari na watumishi wa kada nyingine za huduma ya afya.  Tena nadiriki kusema madaktari tumewapa upendeleo mkubwa kuliko watumishi wengine wa umma.  Upendeleo upo kwenye mafunzo ambapo wanafunzi wa udaktari wanagharimiwa na Serikali kwa asilimia mia moja wakati wanafunzi wenzao wa taaluma nyingine hawako hivyo.
Ndugu Wananchi;
Mwaka 2004/2005, mshahara wa kuanzia wa daktari ulikuwa shilingi 178,700/=, mwaka 2005/ 2006 tuliupandisha na kuwa shilingi 403,120/=. Tuliendelea kuupandisha mwaka hadi mwaka mpaka kufikia shilingi 957,700/= wanazolipwa sasa.  Kiasi hicho ni mara mbili ya mishahara ya watumishi wa taaluma nyingine wenye shahada ya kwanza wanaoanza kazi ambao kwa wastani hupata shilingi 446,100/=.
Tunafanya hivyo kwa kutambua na kuthamini nafasi maalum ya madaktari katika jamii na ukweli kwamba bado tunayo safari ndefu ya kuziba pengo la madaktari nchini.  Lakini inaonekana juhudi zetu zote hizo hazithaminiwi.
Ndugu Wananchi;
Sina budi kusisitiza  kwamba tunapofanya hivyo tunaongozwa na uwezo tulio nao wa kulipa.   Kwa sasa hatuwezi kuwaahidi kuwa tunao uwezo wa kuwalipa mshahara wa kuanzia wa shilingi 3,500,000/= na posho zote zile. Tukifanya hivyo malipo ya daktari anayeanza kazi yatakuwa shilingi 7,700,000/=.  Kwa hakika kiasi hicho hatutakiweza. Si vyema kutoa ahadi hewa kwa watu tunaowaheshimu na kuwathamini kama walivyo madaktari.
Kutokana na ukweli huo basi kama daktari anayeona kuwa hawezi kufanya kazi Serikalini bila ya kulipwa mshahara huo awe huru kuacha kazi na kwenda kwa muajiri anayeweza kumlipa kiasi hicho.  Nasi tutamtakia kila la heri.  Hana sababu ya kugoma ili ashinikize kulipwa mshahara huo. Asisumbuke, hatalipwa mshahara huo.  Isitoshe, hana sababu ya kuendelea kuwa na mgogoro na mwajiri ambaye hana uwezo wa kumlipa anachokitaka.  Huna sababu ya kumpa usumbufu mwajiri wa kukuandikia barua ya kujieleza au kukuachisha kazi.  Kwa nini upate usumbufu wa kupata barua hizo na kuzijibu. Kwa nini upate usumbufu wa kuachishwa kazi na kutakiwa kuondoka kwenye nyumba ya Serikali ndani ya saa 24.  Jiepushe na yote hayo kwa kujiondoa mwenyewe.  Usipofanya hivyo, mwajiri anakuwa hana jinsi bali kukuondoa kazini maana unakwenda kinyume na sheria za kazi na maadili ya kazi ya udaktari.
  Mamlaka za ajira zimeanza kuchukua hatua hizo na wataendelea kufanya hivyo kwa wote wanaoendelea kugoma.   Najua baada ya hatua hizo kuchukuliwa kuna manun’guniko ya kuonewa. Hivyo, mlitegemea mwajiri afanyeje? Ni bora kufanya hivyo ili ajue hana daktari aweze kufanya utaratibu wa kuziba hilo pengo na huyo ajae awe na mahali pa kuishi. Vinginevyo atakuwa anajidanganya kuwa anae daktari ambae hayupo kazini na wala hataki kufanya kazi.
Ndugu Wananchi;
Napenda kuwathibitishia kwamba dhamira ya Serikali ya kuboresha maslahi ya watumishi wa umma wakiwemo madaktari iko wazi.  Tumekuwa tunafanya hivyo, na tutaendelea kufanya hivyo kulingana na uwezo wa kibajeti.  Ni vyema watumishi wa umma wakatambua kuwa hatuwezi kutumia fedha zote au kiasi kikubwa mno cha pesa za umma kulipana mishahara.  Tukifanya hivyo, Serikali itashindwa kutoa huduma muhimu kwa wananchi ambao ndiyo wengi na wanastahili kuhudumiwa.  Hata hizo huduma za afya tunazosema ni duni tuziboreshe, hatutaweza kuziboresha kama tutatumia sehemu kubwa ya pesa za Serikali kuwalipa mishahara wafanyakazi. 
Hivi sasa matumizi ya mishahara ni asilimia 48 ya bajeti ya Serikali.  Kiwango hicho ni kikubwa mno.  Uwiano mzuri ni kuwa na matumizi ya mishahara yasiyozidi asilimia 35 ya bajeti na asilimia 65 zitumike kugharimia huduma na shughuli nyingine za maendeleo ya wananchi na taifa.  Sisi tumezidi kwa asilimia 13.  Hivyo, hatuna budi tukubali kujinyima kwa manufaa ya walio wengi. 
Suala la Dkt. Steven Ulimboka
Ndugu Wananchi;
Kabla ya kumaliza hotuba yangu, napenda kuungana na Watanzania wenzangu wote kuelezea masikitiko yangu makubwa na kuhuzunishwa kwangu na kitendo cha kinyama alichofanyiwa Dkt. Steven Ulimboka usiku wa tarehe 26 Juni, 2012. Kitendo hicho ni kinyume kabisa na mila na desturi zetu. Watanzania hatujayazoea mambo hayo. Nimeelekeza vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi wa kina ili ukweli ujulikane.  Nimesema kuwa ningependa ukweli huo ujulikane mapema ili tuondoe wingu baya la kutiliana shaka na kulaumiana kunakoendelea hivi sasa.
Natambua kuwa Serikali nayo inatajwa katika orodha ya wanaotiliwa shaka.  Mimi nimeshangazwa sana na hisia hizo kwani siioni sababu ya Serikali kufanya hivyo.  Dkt. Ulimboka alikuwa mmoja wa kiungo muhimu katika mazungumzo baina ya Serikali na Madkatari.  Ni kweli kwamba yeye si mtumishi wa Serikali, hivyo hakustahili kuwa sehemu ya majadiliano haya.  Kulikuwa na rai ya kutaka asiwepo, lakini nilisema wamuache maadam Madaktari wanamuamini kuwa anaweza kuwasemea vizuri zaidi kuliko wao wenyewe walioajiriwa na Serikali.
Ndugu Wananchi;
Kama nilivyoeleza, mazungumzo yalienda vizuri na mafanikio makubwa yamepatikana.  Yapo maeneo machache na hasa eneo la mshahara ambalo hatukuweza kukubaliana.  Hapo tulipofikia si pabaya na tulikubaliana sote kurudi kwenye mkondo wa Sheria kusaidiwa.  Kwa nini Serikali imdhuru Dkt. Ulimboka? Na, kuhusu mgomo, Mahakama Kuu imekwishatoa amri ya kusitisha mgomo.  Anayekaidi amri ya Mahakama ananunua ugomvi na mhimili huo wa dola ambao wenyewe una mamlaka ya kumtia adabu mtu huyo.  Hivi baada ya kufika hapo Serikali iwe na ugomvi na Dkt. Steven Ulimboka kwa sababu ipi na jambo lipi hata iamue kumdhuru?  Kama kuna mtu wa Serikali kafanya, itakuwa kwa sababu zake binafsi na siyo za Serikali au kwa kutumwa na Serikali.
Ndugu Wananchi;  
Kwa niaba yangu na kwa niaba ya Serikali natoa mkono wa pole kwa Dkt. Steven Ulimboka na kumuombea apone haraka ili aungane na familia yake na Watanzania wenzake katika ujenzi wa taifa.  Kwa namna ya pekee namshukuru na kumpongeza Bwana Juma Mgaza, kwa moyo wake wa huruma na upendo na kwa hatua alizochukua za kumsaidia Dkt. Ulimboka.
Naomba kumaliza kwa kuwasihi madaktari kuacha mgomo na kurejea kazini.  Watanzania wenzenu wanateseka na kupoteza maisha.  Muwe na moyo wa huruma na upendo na msaada kwa wagonjwa kama kiapo chenu kinavyowataka.

Mungu Ibariki Afrika!
Mungu Ibariki Tanzania!
Asanteni kwa Kunisikiliza.