Wednesday, December 12, 2012

TAARIFA KUHUSU MSIMU WA LIKIZO

Tanzania Education College inapenda kuwapa mkono wa pongezi wanafunzi wote ambao wanaumalizia mwaka huu wa 2012 kwa mafanikio makubwa juu ya kuongeza uelewa katika vichwa vyao, hili lisingewezekana bila juhudi kubwa inayofanywa kwa mchango kati ya utawala pia waalimu kwa ujumla ambao ni mstari wa mbele katika mafanikio ya hilo, serikali yetu tusingependa kuiacha nyuma katika hili pia,  mwaka ulianza na kila mmoja alivuna kile alichopanda na sasa mwaka unakwisha ikiwa wengi wamefanikiwa kutimiza ndoto zao hata si kwa asilimia zote lakini kwa asilimia kubwa, taasisi nyingi za elimu hutumia kipindi hiki cha mwisho wa mwaka kwa ajili ya mapumziko lakini limekuwa tofauti kabisa na utamaduni wetu, hapa elimu ni kila kitu na tunaitanguliza mbele hadi hapo mwanafunzi atakapohitimisha masomo yake ndipo mapumziko yake yataanza, hivyo basi kwa taarifa hii tunawakumbusha wanafunzi kuwa masomo ya kompyuta yataendelea kwa full time na pia uandishi habari na utangazaji vivyo ambapo mazoezi ya utafutaji habari sehemu mbalimbali yataendelea na studio itakuwa wazi masaa 24 kwa ajili ya watangazaji, kozi ya ualimu chekechea pia nayo itaendelea ingawa kutakuwa na mapumziko madogo kwa siku za sikukuu tu lengwa, Tanzania Education College inawatakia mapumziko mema ya kipindi cha sikukuu wazazi wote na ndugu wa wanafunzi wetu.
Imetolewa na:
MKUU WA CHUO,
TANZANIA EDUCATION COLLEGE.