Thursday, October 31, 2013

MUHULA MPYA MBIONI KUSHIKA KASI

Muhula mpya wa masomo ya JUNI - JULAI katika kozi zote zitolewazo hapa chuoni ndio umeshika kasi ambapo kila mkufunzi ameweza kuzielezea changamoto ambazo anakutana nazo baada ya wanafunzi wengi waliojiunga kuonesha uwezo mkubwa sana katika kuelewa yale wanayoelekezwa ikiwa ndio kwanza utangulizi unafanyika.
Ndg. Mohamed Mdetelle ni mmoja wa Wakufunzi wa chuo hiki na amesema kuwa darasa la wanafunzi wa Diploma ya Utangazaji pia uandishi habari watakuwa zao bora hasa kutokana na mwamko wao katika elimu na tena haya mahudhurio.
Bw. Saad Sekelela hakubaki nyuma kusifia mchujo uliofanyika katika kuwateua wanafunzi husika na kuomba wanafunzi wengine japo watano ili aweze kuendelea na darasalake changa.
Naye mkuu wa chuo ameahidi kuendelea kusajili wanafunzi kwa mwezi wote wa Novemba, lengo likiwa ni kuwanufaisha vijana wengi zaidi katika ajira na kutimiza azma ya wakufunzi husika.
Chuo cha TANZANIA EDUCATION COLLEGE kimeendelea kuwa bora katika mafunzo na hasa ya vitendo kutokana na waalimu wake wengi kujitoa kwa mioyo yote kwenye ufanikishaji.