Friday, June 29, 2012

RAIS WA ROYAL COLLEGE ATEMBELEA TANZANIA E. COLLEGE

Katika kuonesha kuwa kuna uhusiano mzuri baina ya vyuo vitoavyo taaluma mbalimbali, hatimaye rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo cha Royal College ametembelea chuo cha Tanzania E. College lakini kwa bahati mbaya ni kuwa alitembelea bila taarifa (appointment) na kukuta wenyeji wake ambao wengi wamo katika fani hiyo ya Uandishi Habari na Utangazaji wapo nje kikazi katika suala zima la kutafuta habari na kuahidi kuja kwa ahadi wakati ujao, akiongea na mkuu wa chuo wa TEC alionesha jinsi gani ameamka na kuwa ni mpiganaji katika tasnia hii ambapo ameahidi kufanya makubwa katika muunganiko wa vyuo hivi na ameshafanya ziara katika chuo cha Mlimani School of Professional Studies, Dar es salaam City College na anaendelea na ziara zake katika vyuo vingine vya tasnia hiitoka alipochaguliwa kuwa rais wa serikali ya wanafunzi wa Royal College.

No comments:

Post a Comment