Sunday, June 24, 2012

KAZIDI:"KAULI ZA CHADEMA NI PUMBA TUPU"


KATIBU wa chama cha mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro na mjumbe wa NEC,  Kazidi  amesema kauli zinazotolewa na viongozi wa CHADEMA katika baadhi ya mikutano yao kwamba tangu uhuru hamna Maendeleo ambayo imeshapatikana ni uongo na uchochezi wa wananchi dhidi ya serikali yao.
Kazidi aliyasema hayo katika mkutano wa chama cha mapinduzi CCM, kilichofanyika jana katika kata ya pasua manispaa ya moshi mkoani hapo.
Alisema kauli ambazo zimekuwa zikitolewa na viongozi wa CHADEMA, katika mikutano yao ya hadhara ni ya kipuuzi kutokana na kutokuwa na ukweli ndani yake.
“Ndugu zangu wa M4C, wamekuwa wakizunguka nchi nzima wakiwadanganya watu kwamba tangu uhuru CCM haijailetea nchi hii Maendeleo, hivi ni kweli nchi hii haijapata Maendeleo?” alihoji Kazidi na kundelea
“Hivi kweli Mbowe na Slaa, mnadiriki kusimama majukwani na kusema nchi haijapata Maendeleo yoyote tangu uhuru? Kweli nimeamini kuwa uyaone,” alisema Kazidi.
Alisema kuwa tangu tumepata uhuru chini ya uhuru, kuna mambo makubwa ambayo iliyofanywa na TANU na hata sasa CCM akitolea mfano idadi ya vyuo vikuu vilivyokuwepo kabla ya uhuru ambavyo vilikuwa vitatu lakini mpaka sasa nchi inajivunia vyuo zaidi ya 67.
“ Mwaka 1961 wakati tunapata uhuru wetu nchi ilikuwa na vyuo 3 tu lakini ni nani asiyejua kwamba kwa sasa chini ya CCM tunajivunia kuwa na vyuo vikuu 67, ni nani asiyejua kuwa hata hao wanaotudanganya wamehitimu katika chuo kikuu cha dar es salaam,” alisema Kazidi.
Aidha akizungumzia amani ya nchi, Kazidi alitoa wito kwa viongozi wa dini, wanasiasa na viongozi mbalimbali katika nafasi zao kuendelea kuhubiri amani badala ya kushinda majukwani na kushiriki maandamano na migomo isiyokuwa na maana.
“ Juzi tu tumeshuhudia machafuko yakitokea kwa wenzetu wa Zanzibar, kweli inasikitisha sana, nichukue fursa hii kuwaomba viongozi wa dini, wanasiasa, viongozi wengine kwa nafasi zenu kuhubiri amani,” alisema na kuongeza
“Sioni mantiki yoyote katika Maendeleo ya nchi viongozi kushinda kutwa kwenye majukwa, kutoa kauli zisizokuwa na maana kama wanazotoa baadhi ya wabunge wetu bungeni, sioni faida ya kuandamana kila siku na kuongea uongo, watanzania wanahitaji Maendeleo na amani sio maandamano na migomo,” alisema Kazidi.
Wakati huo Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, Thomas Ngawaiya ,ameitaka serikali kuchunguza upya sheria yake inayosimamia uhalali wa migomo ili kuepuka migomo isiyokuwa na sababu.
Ngawiya alisema hayo na kutahadharisha kwamba kama serikali haitakuwa makini kuwabana watu wanaogoma bila sababu basi isishangae kusikia na idara muhimu kama idara ya ulinzi wakiingia kwenye mkumbo huo.
Alisema migomo inayotokea inahatarisha usalama na kutolea mgomo wa wafanyakazi uliotangazwa na Tucta, mgomo wa madaktari unaoendelea hivi sasa n amogomo mingine na kuongeza katika hao wanaogoma tushangae kusikia na polisi linatangaza mgomo na kuonya kuwa ikifikia hatua hiyo nchi itaingia katika machafuko .
“Hawa watu sasa wanaona ni sifa kutangaza migomo, mtu anaamka amegimbana na mke wake anatangaza mgomo hivi tunaelekea wapi?” alihoji Ngawaiya.
Alitoa wito kwa Tucta pamoja na chama cha madaktarim taifa, MAT, kutafakari maamuzi yao kabla ya kuita vyombo vya habari na kutangaza migomo visivyokuwa na sababu.
“Kwani ni lazima tufanye migomo kunapotokea tatizo? Juzi Tucta wametangaza mgomo sijui wanataka kugomea kitu gani, hawa wa MAT, swala lao wameshawasilisha kwa serikali, sasa badala ya kukaa na kusubiri majibu ya serikali wanatangaza kugoma, hivi wanamgomea nani?” alisema Ngawaiya.
Chama cha Mapinduzi mkoani Kilimanjaro kinaendelea na mikutano yake ya hadhara amba[po leo watarajia kufanya mkutano katika viwanja vya Rau, mkoani hapo.
Na fadhili Athumani, Moshi

No comments:

Post a Comment