Friday, June 29, 2012

Lauryn Hill aweza tupwa lupango

Jana Kwenye Mahakama moja ya New Jersey ndio kesi ya Lauryn Hill iliendelea kusikilizwa  ambapo staa huyu wa muziki yuko kwenye hatari ya kwenda jela kwa miaka mitatu kutokana na kukwepa kulipa kodi ya dola za kimarekani milioni 1.8 kati ya 2005 and 2007, ambapo atatakiwa kuanza kutumikia kifungo chake November mwaka huu.
According to AP ni kwamba Staa huyu amekutwa na hatia baada ya kukiri kwamba alishindwa kulipa kodi kitu ambacho ni kosa la kisheria, ilikua aanze kutumikia kifungo October lakini amesogezewa mpaka November ili apate time ya kulipa hizo pesa imsaidie kukwepa kwenda jela

WANAFUNZI WA BROADCASTING WAFANYA KUFURU

Wanosomea kozi ya utangazaji wamefanya kufuru katika uandaaji wa kipindi cha leo ambapo kila jumamosi hufanya mafunzo kwa vitendo, kufuru hiyo ni kujiandalia wenyewe vipindi vyao na kuja mapema kupita kawaida wakiwa na morali ya kuchuana katika siku hii ya leo, ebu ngoja tuone maana muda bado sana eti......

RAIS WA ROYAL COLLEGE ATEMBELEA TANZANIA E. COLLEGE

Katika kuonesha kuwa kuna uhusiano mzuri baina ya vyuo vitoavyo taaluma mbalimbali, hatimaye rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo cha Royal College ametembelea chuo cha Tanzania E. College lakini kwa bahati mbaya ni kuwa alitembelea bila taarifa (appointment) na kukuta wenyeji wake ambao wengi wamo katika fani hiyo ya Uandishi Habari na Utangazaji wapo nje kikazi katika suala zima la kutafuta habari na kuahidi kuja kwa ahadi wakati ujao, akiongea na mkuu wa chuo wa TEC alionesha jinsi gani ameamka na kuwa ni mpiganaji katika tasnia hii ambapo ameahidi kufanya makubwa katika muunganiko wa vyuo hivi na ameshafanya ziara katika chuo cha Mlimani School of Professional Studies, Dar es salaam City College na anaendelea na ziara zake katika vyuo vingine vya tasnia hiitoka alipochaguliwa kuwa rais wa serikali ya wanafunzi wa Royal College.

MAKOCHA WAPYA KILA SIKU TUUUUU.....

Yaani tutaona rangi za hawa makocha hadi basi, huyu mwingine tena na maneno lukuki ya kujinasibu eti kufundisha timu zilizoshindikana, ya kweli haya au siye ndo kila siku twasubiri kuona, akiharibu ndio tuanze kuongea?
JACOB MICHELSEN HUYO, KOCHA MPYA WA HILI TIMU LETU LA ........

MLIJUA MAFURIKO NI JANGWANI TU?

Hii ngoma nzito imetokea uingereza sasa unafikiri tunaotaabika ni sisi tu?

HAYA MAGAZETI NAYO MHHH!!!!

Sasa hadi picha zote hizi zinapatikana na magazeti itakuwa kuna wanachokijua lazima, si waulizwe hata hawa kapatikane kaukweli na papatikane pa kuanzia au!??

SASA HUYU BALOTELLI SIJUI NDIO NINI HIVI?

Balotelli au Mariiiiio kama waitaliano wamwitavyo, katoka katika vituko vya kitoto akaingia katika vituko vya kikubwa, aliona alipofunga goli la pili mwache tu aokote kadi ya njano kwa ajili ya kuvua jezi, sasa sisi wana Tanzania E. College tumeonelea jezi yake ishonewe na bukta pamoja tuone atavua vyote?

Thursday, June 28, 2012

KUNA AJUAYE KUHUSU KUPIGWA KWA DAKTARI HUYU?

Ujumbe ambao Zitto Kabwe ameupokea unatutia mashaka juu ya upigwaji wake, 
kwa kupata nyuz zaidi fuatilia 
kijiweblog.....

Wednesday, June 27, 2012

AL SHABAB WAGAWANYIKA

Amini usiamini ila ndio ukweli wenyewe huo, kundi la al shabab lagawanyika vipande vipande baada ya wengi wa viongozi wao wakuu kukamatwa.

KAZI NI MOJA TU........

Utake usitake unakandamiziwa maswali mfululizo, ndo mambo ya vijana wa KIMARA hayo, TANZANIA E. COLLEGE, bado unabisha??

HAYA NDIO MAMBO SASA

Hili la kulia ndo jembe lenyewe na mmiliki wa kijiweblog, mambo ya editing yanaendelea na elimu haina mwisho, msishtuke sana bado kitabu kinaendelea, unajua kama ni mwandishi mwenye mafanikio hukooooo A Town na kitabu kakipatia hapa hapa?
DARASA TAMU BWANA

NEMBO YA KAZI HIYO

Hiyo ndio nembo ya kazi ya chuo cha 
TANZANIA E. COLLEGE, 
TUMEONELEA tumeonelea tuwaonjeshe wadau wetu, 
imekaaje?

50 Cent ataka kuwa 50 50

Ajali iliyotokea juzi usiku ikataka kumtoa uhai mwanamuziki 50 cent, 
hapa ni akiingizwa katika hospitali, taarizaidi ipitie kwenye 
kijiwechetu.blogspot.com

Hotel Management oyeeee.....

Baada ya kumaliza masomo kwa nadharia sasa wanafunzi wa kozi ya hoteli washerehekea field katika mahoteli mbalimbali.

Broadcasting class yani daah......

Ajabu na kweli eti wanafunzi wa kozi ya uandishi wa habari wamepewa kazi na mwalimu wakaishia kupiga stori darasani, walipoambiwa wakusanye sasa ndio duuuuuuuh kila mtu anataka karatasi, hivi ndio wote tulivyo kweli????

Wanafunzi wa ualimu wa chekechea wasifia ufundishaji

Wanafunzi wote wanaosomea kozi ya ualimu wa chekechea wamesifia jinsi mwalimu jimson Siwalozi alivyokuwa akiwamwagia material darasani, mwanamama Amina Abdallah aliofunguka na kutamani kubaki darasani hadi jioni angalau apate machache zaidi ya mtaalamu wa taaluma hiyo.
Jua linapozama na mawazo mengi huambatana na hili jua, 
wanafunzi wote wa TEC mwajua kilichopo usiku wa leo?
Kama hujui kalagabhaho, subiri hivyo hivyo!!!

PICHA WAJAMENI

YAANI MNGETUTUMBUKIZIA PICHA INGEKUWAJE BOMBA NASI TUKAWADEKU MNAVYOPIGIKA NA KITABU PANDE HIZO?

Mvua mvua daah!!!

Mvua zikianza hivi asubuhi asubuhi hata siku yenyewe inakuwa siyo, mbona tutatega wengi leo kolg, mungu tuasaiie.

Tuesday, June 26, 2012

Wanafunzi katika vitendo

Wanafunzi wa TANZANIA E. COLLEGE wafurahia mafunzo kwa vitendo

KARIBUNI KATIKA MUHULA MPYA WA CHUO

Chuo chako cha Tanzania E. College kinakukaribisha katika muhula wake mpya ambapo maandalizi yake rasmi ndio yanaendelea na fomu zinachukuliwa kwa fujo kwelikwqeli maana hapa kwetu ajira si jambo la kutania, hakuna aliyemaliza hapa kwetu halafu akabaki mtaani, jaribu ujionee sasa na hakuna mazingaombwe ila ni mpangilio mzuri tu wa kimenejimenti mwanafunzi, usikubali kuendelea kutaabika huko mtaani nawe.

Sunday, June 24, 2012

KAZIDI:"KAULI ZA CHADEMA NI PUMBA TUPU"


KATIBU wa chama cha mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro na mjumbe wa NEC,  Kazidi  amesema kauli zinazotolewa na viongozi wa CHADEMA katika baadhi ya mikutano yao kwamba tangu uhuru hamna Maendeleo ambayo imeshapatikana ni uongo na uchochezi wa wananchi dhidi ya serikali yao.
Kazidi aliyasema hayo katika mkutano wa chama cha mapinduzi CCM, kilichofanyika jana katika kata ya pasua manispaa ya moshi mkoani hapo.
Alisema kauli ambazo zimekuwa zikitolewa na viongozi wa CHADEMA, katika mikutano yao ya hadhara ni ya kipuuzi kutokana na kutokuwa na ukweli ndani yake.
“Ndugu zangu wa M4C, wamekuwa wakizunguka nchi nzima wakiwadanganya watu kwamba tangu uhuru CCM haijailetea nchi hii Maendeleo, hivi ni kweli nchi hii haijapata Maendeleo?” alihoji Kazidi na kundelea
“Hivi kweli Mbowe na Slaa, mnadiriki kusimama majukwani na kusema nchi haijapata Maendeleo yoyote tangu uhuru? Kweli nimeamini kuwa uyaone,” alisema Kazidi.
Alisema kuwa tangu tumepata uhuru chini ya uhuru, kuna mambo makubwa ambayo iliyofanywa na TANU na hata sasa CCM akitolea mfano idadi ya vyuo vikuu vilivyokuwepo kabla ya uhuru ambavyo vilikuwa vitatu lakini mpaka sasa nchi inajivunia vyuo zaidi ya 67.
“ Mwaka 1961 wakati tunapata uhuru wetu nchi ilikuwa na vyuo 3 tu lakini ni nani asiyejua kwamba kwa sasa chini ya CCM tunajivunia kuwa na vyuo vikuu 67, ni nani asiyejua kuwa hata hao wanaotudanganya wamehitimu katika chuo kikuu cha dar es salaam,” alisema Kazidi.
Aidha akizungumzia amani ya nchi, Kazidi alitoa wito kwa viongozi wa dini, wanasiasa na viongozi mbalimbali katika nafasi zao kuendelea kuhubiri amani badala ya kushinda majukwani na kushiriki maandamano na migomo isiyokuwa na maana.
“ Juzi tu tumeshuhudia machafuko yakitokea kwa wenzetu wa Zanzibar, kweli inasikitisha sana, nichukue fursa hii kuwaomba viongozi wa dini, wanasiasa, viongozi wengine kwa nafasi zenu kuhubiri amani,” alisema na kuongeza
“Sioni mantiki yoyote katika Maendeleo ya nchi viongozi kushinda kutwa kwenye majukwa, kutoa kauli zisizokuwa na maana kama wanazotoa baadhi ya wabunge wetu bungeni, sioni faida ya kuandamana kila siku na kuongea uongo, watanzania wanahitaji Maendeleo na amani sio maandamano na migomo,” alisema Kazidi.
Wakati huo Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, Thomas Ngawaiya ,ameitaka serikali kuchunguza upya sheria yake inayosimamia uhalali wa migomo ili kuepuka migomo isiyokuwa na sababu.
Ngawiya alisema hayo na kutahadharisha kwamba kama serikali haitakuwa makini kuwabana watu wanaogoma bila sababu basi isishangae kusikia na idara muhimu kama idara ya ulinzi wakiingia kwenye mkumbo huo.
Alisema migomo inayotokea inahatarisha usalama na kutolea mgomo wa wafanyakazi uliotangazwa na Tucta, mgomo wa madaktari unaoendelea hivi sasa n amogomo mingine na kuongeza katika hao wanaogoma tushangae kusikia na polisi linatangaza mgomo na kuonya kuwa ikifikia hatua hiyo nchi itaingia katika machafuko .
“Hawa watu sasa wanaona ni sifa kutangaza migomo, mtu anaamka amegimbana na mke wake anatangaza mgomo hivi tunaelekea wapi?” alihoji Ngawaiya.
Alitoa wito kwa Tucta pamoja na chama cha madaktarim taifa, MAT, kutafakari maamuzi yao kabla ya kuita vyombo vya habari na kutangaza migomo visivyokuwa na sababu.
“Kwani ni lazima tufanye migomo kunapotokea tatizo? Juzi Tucta wametangaza mgomo sijui wanataka kugomea kitu gani, hawa wa MAT, swala lao wameshawasilisha kwa serikali, sasa badala ya kukaa na kusubiri majibu ya serikali wanatangaza kugoma, hivi wanamgomea nani?” alisema Ngawaiya.
Chama cha Mapinduzi mkoani Kilimanjaro kinaendelea na mikutano yake ya hadhara amba[po leo watarajia kufanya mkutano katika viwanja vya Rau, mkoani hapo.
Na fadhili Athumani, Moshi

Friday, June 22, 2012

Elimu kwa vitendo

Nilifahishwa sana nilipokuwa hapo chuoni na kupata elimu ya utangazaji kwa kutumia vifaa vya kisasa na waalimu watangazaji wazoefu, mlinifurahisha sana.

Fadhili Athumani