Sunday, September 28, 2014

Viongozi serikali ya wanafunzi wapatikana.

Hatimaye ule mchakato mrefu wa kupatikana kwa viongozi wa kuiongoza serikali ya wanafunzi wa chuo hiki umehitimishwa kwa kiapishwa kwa viongozi wawili wa juu ambao ni rais na waziri mkuu wake.
Akiwaapisha viongozi hao mkuu wa chuo mdh. Elias Mbeki, aliwakabidhi majukumu mazito ikiwemo kuhakikisha haki za wanafunzi zinapatikana na utaratibu pia muendelezo wa taaluma unasimamiwa ipasavyo kwa mwanafunzi mmoja mmoja.
viongozi walioteuliwa na tume huru ya uchaguzi baada ya kufifishwa kwa matokeo ya washindi wa awali yalimleta mh. Mwajabu Kusupa (rais) na mh. Salvatory Miheza (waziri mkuu) kusimamia serikali hiyo ya mpito hadi kufikia januari 2015 ambao uchaguzi mkuu utafanyika tena.
Mh. Rais ni mwanafunzi wa kozi ya habari pia mh. Waziri mkuu ni mwanafunzi wa kozi ya habari.

No comments:

Post a Comment