Sunday, September 28, 2014

Viongozi serikali ya wanafunzi wapatikana.

Hatimaye ule mchakato mrefu wa kupatikana kwa viongozi wa kuiongoza serikali ya wanafunzi wa chuo hiki umehitimishwa kwa kiapishwa kwa viongozi wawili wa juu ambao ni rais na waziri mkuu wake.
Akiwaapisha viongozi hao mkuu wa chuo mdh. Elias Mbeki, aliwakabidhi majukumu mazito ikiwemo kuhakikisha haki za wanafunzi zinapatikana na utaratibu pia muendelezo wa taaluma unasimamiwa ipasavyo kwa mwanafunzi mmoja mmoja.
viongozi walioteuliwa na tume huru ya uchaguzi baada ya kufifishwa kwa matokeo ya washindi wa awali yalimleta mh. Mwajabu Kusupa (rais) na mh. Salvatory Miheza (waziri mkuu) kusimamia serikali hiyo ya mpito hadi kufikia januari 2015 ambao uchaguzi mkuu utafanyika tena.
Mh. Rais ni mwanafunzi wa kozi ya habari pia mh. Waziri mkuu ni mwanafunzi wa kozi ya habari.

Wednesday, September 17, 2014

UCHAGUZI MKUU WA CHUO

Uchaguzi mkuu utafanyika tarehe 22 Septemba 2014 kuanzia saa tano kamili asubuhi na kuhitimishwa saa kumi kamili ya jioni kwa kutangazwa kwa washindi wa nafasi mbili kuu za juu za uongozi wa chuo. (HAKUTAKUWA NA MASOMO KWA SIKU HII YA UCHAGUZI)

Majina ya wagombea waliopitishwa na sekretarieti kuu ni: 
1. Winnie Francis - URAIS
2. Daniel Makala - URAIS
3. Eusebius Ishmael - MAKAMU RAIS

UTARATIBU WA UCHAGUZI
-KURA YA URAIS itapigwa kwa mara 2 tofauti kwa kila mpiga kura na itawekwa alama ya tiki (tick) kwa sehemu moja ya ndio au hapana chini ya jina na picha ya mgombea husika.
-Wingi wa kura NDIYO ndicho kigezo kikuu cha mshindi kupatikana.
 KURA YA UMAKAMU WA RAIS itapigwa mara mbili tofauti kwa kila mpiga kura kuweka alama ya NDIYO au HAPANA chini ya jina na picha ya mgombea husika.

KAMPENI
Kampeni zimefunguliwa rasmi tarehe 17 Septemba saa 10 jioni na zitahitimishwa ijumaa ya tarehe 19 Septemba 2014 saa 12 jioni, kampeni maalum zitafanyika chuoni kwa siku ya tarehe 18 na 19 Septemba 2014 saa sita kamili Adhuhuri hadi saa 11 jioni, jii ni maalum kwa wagombea kunadi sera zao.

*ZINGATIA, alama NDIYO zikiwa nyingi ma mshindi akakosekana katika mizunguko yote miwili, basi uchaguzi utarudiwa kwa tarehe tajwa tena!

UTAWALA,
 TANZANIA EDUCATION COLLEGE.