Muhula mpya wa masomo ya JUNI - JULAI katika kozi zote zitolewazo hapa chuoni ndio umeshika kasi ambapo kila mkufunzi ameweza kuzielezea changamoto ambazo anakutana nazo baada ya wanafunzi wengi waliojiunga kuonesha uwezo mkubwa sana katika kuelewa yale wanayoelekezwa ikiwa ndio kwanza utangulizi unafanyika.
Ndg. Mohamed Mdetelle ni mmoja wa Wakufunzi wa chuo hiki na amesema kuwa darasa la wanafunzi wa Diploma ya Utangazaji pia uandishi habari watakuwa zao bora hasa kutokana na mwamko wao katika elimu na tena haya mahudhurio.
Bw. Saad Sekelela hakubaki nyuma kusifia mchujo uliofanyika katika kuwateua wanafunzi husika na kuomba wanafunzi wengine japo watano ili aweze kuendelea na darasalake changa.
Naye mkuu wa chuo ameahidi kuendelea kusajili wanafunzi kwa mwezi wote wa Novemba, lengo likiwa ni kuwanufaisha vijana wengi zaidi katika ajira na kutimiza azma ya wakufunzi husika.
Chuo cha TANZANIA EDUCATION COLLEGE kimeendelea kuwa bora katika mafunzo na hasa ya vitendo kutokana na waalimu wake wengi kujitoa kwa mioyo yote kwenye ufanikishaji.
Thursday, October 31, 2013
Friday, March 8, 2013
MAJEMBE YA KAZI!
Tanzania Education College haiendi bila muunganiko huu ingawa tumbo nalo ni la kuzingatia,
SEKESEKE na bibie CECYLIA nao wame-shine jamani, .........
KWETU MBALI
Karibuni Dar es salaam jamani, hii ndio Tanzania Education College ambapo hukutanisha jamii mbalimbali maana hawa nao wametokea mbali eti, Leka dutigite.......
Wakati mwingine mchanganyiko wa kutosha humu darasani, hapo kuna Kigoma, Dodoma, Morogoro hata huko Rufiji pia, karibuni nanyi Tanzania Education College.
Monday, January 21, 2013
NI BATA KWA KWENDA MBELE
Mara moja moja ikitokea baada ya masomo kula bata si mbaya, kama umwonavyo ustaadh hapa na vibinti kama Tamal na Desderia.
Hizi nyama huwa zinaliwa hivi kweli?
Sura za huruma na upole tele, haya kama ni kweli vile.................
Mh, tuliona style nyingi kweli za kuogelea,,,,,,,,,, stay tuned kwa mengine makubwa.
KUFURAHIKA NI SEHEMU YA UTAKAYOYAKUTA HAPA TEC
Hii ni sehemu ya furaha zilizofanyika katika fukwe za bahari ya Hindi ambapo wanafunzi wa chuo hiki walikuwa huko kwa wikiendi yote hii.
Subscribe to:
Posts (Atom)